Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trump afuta haki ya uraia wa kuzaliwa kwa wahamiaji haramu, wenye viza za muda

Muktasari:

  • Marekebisho ya 14 ya Katiba ya Marekani, yaliyopitishwa zaidi ya karne moja iliyopita, yamekuwa msingi wa uamuzi wa Mahakama ya Juu yanayowalinda watoto wa wazazi wa kigeni waliozaliwa nchini Marekani.

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesaini amri kadhaa za kiutendaji baada ya kuapishwa, ikiwemo kufuta haki ya uraia wa kuzaliwa kwa watoto wa wahamiaji haramu na wenye viza za muda.

Uamuzi huu umebadilisha tafsiri ya muda mrefu ya marekebisho ya 14 ya Katiba ya Marekani, ambayo yalikuwa yakitoa uraia wa kuzaliwa kwa yeyote aliyezaliwa nchini Marekani, bila kujali hali ya kisheria ya wazazi wake.

Kwa mujibu wa amri hiyo mpya, watoto waliozaliwa Marekani hawatatambuliwa kama raia wa nchi hiyo iwapo wazazi wao ni wahamiaji wasio halali au wana viza za muda.

Hatua hiyo itaanza kutekelezwa siku 30 kutoka sasa, na watoto watakaozaliwa nchini humo watahitajika kuwa na angalau mzazi mmoja ambaye ni raia wa Marekani au mkazi wa kudumu mwenye kadi ya kijani.

Marekebisho ya 14 ya Katiba ya Marekani, yaliyopitishwa zaidi ya karne moja iliyopita, yamekuwa msingi wa uamuzi wa Mahakama ya Juu yanayowalinda watoto wa wazazi wa kigeni waliozaliwa nchini Marekani.

hivyo, Trump ameenda kinyume na uamuzi huo, akisisitiza kuwa sheria za sasa zimekuwa zikivutia wahamiaji haramu kuingia nchini humo.

Aidha, Trump ametia saini amri nyingine inayolenga wahamiaji haramu waliopatikana na hatia za makosa makubwa ya jinai.

Kwa mujibu wa amri hiyo, wahamiaji hao sasa watakabiliwa na adhabu ya kifo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupambana na uhalifu unaodaiwa kusababishwa na wahamiaji wasio halali.

Hatua hizo zimeibua mjadala mkali miongoni mwa wanaharakati wa haki za binadamu na wataalamu wa sheria, wakisema kuwa mabadiliko hayo yanakwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu na Katiba.

Baadhi ya wakosoaji wamedai kuwa sera hizi mpya zinaweza kuongeza mgawanyiko wa kijamii na kushusha hadhi ya Marekani kama nchi yenye historia ya kukaribisha wahamiaji.