Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tinubu atangazwa Rais mteule Nigeria

Bola Tinubu, Rais mteule wa wa Nigeria kwa tiketi ya chama tawala cha APC.

Muktasari:

  • Mgombea wa urais kwa tiketi ya chama tawala cha APL nchini Nigeria, Bola Tinubu ameibuka mshindi baada Tume ya Uchanguzi kumtangaza mshindi kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Jumamosi.

Abuja. Tume ya uchaguzi, INEC, imemtangaza Bola Tinubu, mgombea wa chama tawala cha Nigeria, APC, kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi.
Tinubu aliwashinda wagombea wengine 17 walioshiriki uchaguzi huo.

Tinubu amepata jumla ya kura 8,794,726, idadi kubwa zaidi ya wagombea wote, hivyo kukidhi matakwa ya kwanza ya kikatiba ya kutangazwa mshindi.

Pia alipata zaidi ya asilimia 25 ya kura zilizopigwa katika majimbo 30, zaidi ya majimbo 24 yanayohitajika kikatiba.

Mwenyekiti wa INEC Mahmood Yakubu, ambaye ametangaza matokeo ya mwisho mapema leo Jumatano mjini Abuja, amesema Atiku Abubakar wa PDP alishika nafasi ya pili katika uchaguzi huo.

Atiku amepata jumla ya kura 6,984,520 katika uchaguzi huo huku Peter Obi wa Chama cha Labour akiibuka wa tatu katika uchaguzi huo kwa jumla ya kura 6,101,533 huku Rabiu Kwankwaso wa NNPP akiibuka wa nne kwa kura 1,496,687.

Yakubu amesema cheti cha Rais na Makamu wa Rais kitatolewa leo Jumatano katika Kituo cha Kitaifa cha Ukusanyaji wa kura.
Wagombea wanne pekee ndio walioshinda uchaguzi wa urais katika angalau jimbo moja.
Hata hivyo, kushinda majimbo mengi si sharti kwa mgombea kutangazwa mshindi wa uchaguzi.