Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruto aapa kukomesha maandamano Kenya

Rais wa Kenya, William Ruto.

Muktasari:

  • Kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga anaongoza maandamano nchini humo kupinga utawala wa Rais William Ruto pamoja na hali ngumu ya maisha wanayopitia wananchi hasa wa hali ya chini.

Kenya. Rais William Ruto amesema hataruhusu kiongozi wa Azimio la Umoja, Raila Odinga kutumia damu za Wakenya kujipatia madaraka huku akisema hawezi kuruhusu maandamano hayo kuendelea nchini humo.

Akizungumza mjini Naivasha leo Ijumaa Julai 14, 2023, Rais Ruto amesema atatumia mbinu zote kuhakikisha kuwa anakomesha maandamano hayo ya upinzani nchini humo.

“Raila Odinga, sitakuruhusu kutafuta madaraka kwa mgongo wa damu za Wakenya. Nitakuzuia,” amesema.

Rais Ruto ameyasema hayo alipokuwa akijibu tangazo la Azimio la Umoja kwamba maandamano yao yajayo yatafanyika kwa siku tatu mfululizo, kuanzia wiki ijayo.

Amemtaka Odinga kuacha kutumia njia zisizo za kikatiba kuingia madarakani huku akisisitiza kwamba hilo halitafanikiwa.

Rais Ruto amesisitiza msimamo wake kuwa hakutakuwa na maridhiano kati ya serikali yake na upande wa upinzani.

“Huwezi kutumia njia zisizo za kikatiba kupata madaraka. Unataka kutumia vurugu kuingia serikalini; hautafanikiwa,” ameongeza Ruto akimlenga Odinga.

Rais Ruto amemtuhumu Odinga kwamba ameleta machafuko nchini humo ambayo yamesababisha vifo vya watu 12 huku akisema amezoea kufanya hivyo tangu utawala wa Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta.

Takriban vifo 12 vilirekodiwa katika maandamano ya Jumatano Julai 12, 2023 nchini humo.  Azimio la Umoja wamepanga kuendelea na maandamano hayo kwa siku tatu mfululizo kuanzia Jumatano hadi Ijumaa huku kiongozi wa Azimio, Odinga akisema maandamano hayo yatafanyika hata kama Serikali haitatoa kibali.