Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruto amtuhumu Kenyatta kufadhili maandamano Kenya

Rais wa Kenya, William Ruto

Muktasari:

  • Siku chache baada ya maelfu ya wananchi kuandamana, Rais wa Kenya William Ruto ametuhumu Rais mstaafu nchini huko Uhuru Kenyatta kufadhili maandamano ya upinzani nchini humo.

Kenya. Rais wa Kenya, William Ruto amemtuhumu mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta kuwa anafadhili maandamano ya upinzani nchini humo.

Akizungumza huko kaunti ya Nakuru leo Julai 14, 2023, Rais Ruto amedai kuwa Kenyatta alikuwa akiwafadhili vijana wa Mungiki kufanya fujo wakati wa maandamano ya Azimio la Umoja nchini humo.

Rais Ruto ameonya kuwa ikiwa Rais huyo wa zamani ataendelea kufadhili shughuli za Azimio, atalazimika kumchukulia hatua.

Amemtaka Kenyatta kuwa muungwana, akisema kuwa yeye alimuunga katika kipindi akiongoza nchi hiyo.

Pia, Rais Ruto amemtaka Kenyatta kuacha kujihusisha na kiongozi wa ODM, Raila Odinga.

“Nikuombe rafiki yangu Uhuru, achana na huyo mzee (Raila), acha kutoa pesa za kuajiri mungiki kuiharibu Nairobi, wewe ulikuwa Rais tukakuunga mkono, tafadhali kuwa muungwana,” amesema Rais Ruto.