Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Mujica anayetajwa kuwa maskini zaidi duniani afariki dunia

Rais wa zamani wa Uruguay, Jose "Pepe" Mujica enzi za uhai wake. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Kilichomuua Pepe Mujica, ni ugonjwa wa saratani ya umio, iliyogunduliwa Mei 2024 na kutibiwa kwa upasuaji mara mbili Septemba na Desemba 2024. Kutokana na ugonjwa huo, afya yake ilizidi kuzorota na kuwa dhaifu kila kukicha jambo lililomfanya aombe kusitishiwa matibabu yote mwanzoni mwa Januari, mwaka huu hadi alipofariki dunia.

Uruguay. Rais wa zamani wa Uruguay, Jose "Pepe" Mujica amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89.

Rais Mujica ambaye anasifika na kutambulika kama ‘Rais maskini zaidi duniani’ kabla ya kukalia kiti cha urais (2010-2015) alikuwa mpiganaji wa zamani wa msituni aliyegeuzwa na demokrasia ya kijamii. Pia alijizolea umaarufu kutokana na msimamo wake wa kutopenda kuonekana kwenye vyombo vya habari.


Tukio la mara ya mwisho kwake kuhudhuria hadharani lilikuwa la kuapishwa kwa rais mpya wa Uruguay, Yamandu Orsi, Machi 1, mwaka huu, akiwa ameketi pamoja na marais wa zamani, Luis Alberto Lacalle Herrera (1990-1995) na baba yake rais aliyeongoza taifa hilo kati ya mwaka, 1985-1990, Julio Sanguinetti.

Kwa mujibu wa Al Jazeera, Mujica alikuwa rais kipenzi cha wananchi wote wa Uruguay kutokana na maisha yake ya kutopenda kujilimbikizia mali na kutamani kuona wananchi wake wakifurahia rasilimali za taifa lao.

"Simba mzee alikuwa amefunga pazia mapema kidogo, Nataka kufa kwa amani, hakuna ziara tena, hakuna mahojiano tena,’ aliwahi kunukuliwa Pepe Mujica, wakati akiwaaga raia wake na kuachia madaraka.


Baada ya kustaafu, Mujica alirejea kwenye shamba lake dogo lililoko Rincón del Cerro, jijini Montevideo nchini humo.

Uamuzi wake wa kujichimbia kwenye shamba lake huku akiishi kwenye nyumba ya kawaida, uliwalazimu baadhi ya watu maarufu na mashuhuri waliohitaji kuonana naye kwenda hukohuko alikokuwa akiishi. Miongoni mwa watu waliokuwa wakimtembelea ni pamoja na Aerosmith, Sean Penn, Glenn Close, Ricky Martin, Milton Nascimento na wengine wengi.

Januari, wasanii wa Hispania na Amerika Kusini, Joaquin Sabina, Silvio Rodriguez, Leon Gieco, walitunga wimbo unaoitwa ‘Una canción y unas palabras para Pepe’, kuenzi utendaji kazi wake.

Mbali na wasanii hao, mtengenezaji wa filamu maarufu nchini Serbia, Emir Kusturica alirekodi filamu na rais huyo kwa miaka mitatu iliyoitwa ‘El Pepe, una vida suprema’, ambayo baadaye ilionyeshwa kwenye mtandao wa Netflix.

Pepe Mujica alihitimisha safari yake ya kisiasa, baada ya muhula wa urais (2010-2015).

Kutokana na tishio la Uviko-19, Mujica aliibuka na kusema:  "Mimi ni mzee na ninaugua ugonjwa sugu wa kinga.”


Kilichomuua

Kwa mujibu wa Al Jazeera, kilichomuua Pepe Mujica, ni ugonjwa wa saratani ya umio, iliyogunduliwa Mei 2024 na kutibiwa kwa kufanyiwa upasuaji mara mbili kati ya  Septemba na Desemba 2024,

Kutokana na ugonjwa huo, afya yake ilizidi kuzorota na kuwa dhaifu kila kukicha jambo lililomfanya aombe kusitishiwa matibabu yote mwanzoni mwa Januari, mwaka huu hadi alipofariki dunia.

Rais wa ajabu

Pepe Mujica akiwavutia wasanii wa filamu na muziki, pia alipendwa sana na wanahabari na waandishi wa vitabu.

Vitabu vingi kumhusu vimeandikwa kikiwamo cha mwanahabari, Andres Danza na Ernesto Tulbovitz, ambao walichapisha kitabu mwaka wa 2015, kinachojumuisha mahojiano na Pepe Mujica kilichoitwa ‘Pepe Mujica: Kondoo Mweusi Aliye Madarakani.’

Katika kitabu hicho, waandishi hao kwenye utangulizi, wanakumbusha umaarufu wa kimataifa wa rais Pepe Mujica. Ni Rais wa ajabu ambaye alikataa kuhamia katika ikulu ya rais, ambaye alitoa asilimia 90 ya mshahara wake kwenda shirika la makazi ya kijamii, ni Rais ambaye alikuwa na magari mawili tu ya zamani.


Imeandikwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa mashirika ya habari.