Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Odinga atoa taarifa polisi jaribio la mauaji dhidi yake

Muktasari:

  • Kufuatia kupigwa risasi kwa gari ya kiongozi wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga katika maandamano Alhamisi iliyopita, kiongozi huyo amewasilisha malalamiko yake polisi akidai lilikua jaribio la kumuua.

Dar es Salaam. Kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga amewasilisha malalamiko yake rasmi kwa Polisi kuhusu jaribio la mauaji.

Odinga kupitia kwa wakili wake Jackson Awele, alidai kuwa kuna uwezekano kuwa maofisa wa polisi walikuwa wakiendesha kazi chini ya amri ya Inspekta Jenerali wa Polisi na kwamba Serikali ilijaribu kumuua kabla.

Kwa mujibu wa mtandao wa uzalendo wa nchini humo, tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita saa 4:30 asubuhi, huku Raila na viongozi wake wa Azimio wakiongoza waandamanaji huko Pipeline.

Katika barua kwa Afisa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kware, Odinga aliwataka polisi wahifadhi malalamiko hayo katika Kitabu chao cha Matukio na apewe namba ya kuingia na maelezo zaidi.

Kiongozi huyo wa upinzani alisema kwa ushirikiano wa wananchi kwa ujumla wamewatambua maofisa wawili wa utumishi Namba 88011 Koplo Kemboi na Utumishi Namba 226944 Konstebo Ndirangu.

"Wakati wa ghasia hizo, maofisa wa polisi walikaribia gari la Raila na kulimiminia takriban risasi kumi za moto." "Uchunguzi uliofuata wa gari kufuatia shambulio hilo unaonyesha kuwa gari hilo lililengwa kwa makusudi, huku mteja wetu akiwa mlengwa halisi," wakili huyo alisema.

"Kuna sababu ya kuamini kwamba maofisa wanaofanya kazi kwa amri ya Inspekta Jenerali wa Polisi na Serikali, kwa nia mbaya, walijaribu kufanya uhalifu, kusababisha kifo cha mteja wetu," wakili huyo aliongeza.

Raila alisema kuwa siku husika, majira ya saa 4:30 asubuhi, wakati wa msafara wake, walikutana na kundi la maafisa wa polisi waliokuwa wamejihami wakiwa wameegemea upande uleule maandamano yasiyokuwa na vurugu yalipokuwa yakiandamana.