Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muuza barakoa aliyepigwa risasi kwenye maandamano afariki

Muktasari:

  • Kijana huyo kutoka Nairobi aliyejulikana kwa jina Boniface Kariuki alionekana kwenye kipande cha video akipigwa risasi kichwani na polisi kwa karibu akiwa katika moja ya mtaa wa jiji hilo.

Dar es Salaam. Taarifa kutoka nchini Kenya zinasema kijana muuza barakoa aliyepigwa risasi kwenye hekaheka za maandamano ya Juni 17, 2025 amefariki dunia.

Kijana huyo kutoka Nairobi aliyejulikana kwa jina Boniface Kariuki alionekana kwenye kipande cha video akipigwa risasi kichwani na polisi kwa karibu akiwa katika moja ya mtaa wa jiji hilo.

Vyombo vya habari vya BBC, NTV na Nation Africa vimeripoti kifo hicho vikimnukuu msemaji wa familia Emily Wanjira ya kwamba Kariuki amefariki jana Jumatatu usiku saa 3:15.

Tofauti na maandamano ya Juni 25, 2025 ya kumbukizi ya vifo vya watu 60 waliouawa mwaka jana 2024 kwenye maandamano ya Gen-Z, Kariuki yeye alipigwa risasi kwenye maandamano ya kutafuta haki kwa mwanahabari Albert Ojwang aliyefariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi jijini humo.

Tangu siku hiyo ya Juni 17, Kariuki kupigwa risasi, alikuwa amefanyiwa upasuaji mara mbili katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta ambapo alilazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

“Kariuki mwenye umri wa miaka 22 hayuko tena nasi, ameacha ndugu watatu na wazazi wake” amesema Wanjira,

Imelezwa madaktari waliokuwa wakimhudumia katika hospitali alikokuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa majuma mawili waliiambia familia yake kuwa ubongo umekufa na saa kadhaa baadaye kuwathibitishia kuwa amefariki dunia.

Kwa mujibuwa BBC kufa kwa ubongo kunatambuliwa kisheria na kiafya kama kifo nchini Kenya.


Familia yasikitishwa

Baada ya kifo chake familia imesikitishwa katika kile ilichodai marehemu ndiye aliyekuwa na makosa baada ya aliyekuwa msemaji wa polisi, Charles Owino, kusema alikuwa na makossa.

Owino aliwashangaza Wakenya kutokana na matamshi yake alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha asubuhi cha Citizen TV.

“Kariuki alipigwa risasi na ofisa wa polisi kwa sababu alimkosea heshima kwa kumtukana, jambo ambalo lilimchochea. Ukiisikiliza video kwa makini, utamsikia Boniface akimwambia polisi,” amesema.

Hata hivyo, Owino alikiri kwamba ofisa huyo hakupaswa kujibu kwa kumpiga risasi kijana huyo, kwani alipaswa kuonyesha uvumilivu.

Pia, Msemaji wa familia Wanjira, ameshangaa ni kwa nini Owino ametoa madai hayo kujaribu kuhalalisha kifo cha mpendwa wao. Alisema si njia sahihi ya kushughulikia suala hilo, kwani kijana wao alikuwa anauza barakoa tu na hakuwa hata akishiriki maandamano