Mchekeshaji aunasa urais Ukraine

Muktasari:
- Awamu ya kwanza alishinda kwa asilimia zaidi ya 30 za kura ambapo zilikuwa ni mara mbili ya mpinzani wake Poroshenko ambaye alikuwa na asilimia 15
Ukraine. Mchekeshaji asiye na uzoefu wa kisiasa, Volodymyr Zelensky, ameshinda ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa rais nchini Ukraine Jumapili na kupongezwa na viongozi duniani kote.
Kura hizo zimempa nafasi mwanasiasa mpya ambaye amechaguliwa kwa kuungwa mkono na zaidi ya asilimia 70.
Zelensky (41) ameweza kumtoa madarakani Rais Petro Poroshenko ambaye amekubali kushindwa.
Matokeo ya sasa yanaonekana kuwa ni pigo kubwa kwa Poroshenko na kukataliwa kuanzishwa kwa Ukraine mpya.
"Sitawaangusha," Zelensky aliwaambia waliomuunga mkono wakati wa sherehe za kujipongeza.
Aliongeza kwa kusema: "Sijawa rais bado lakini kama raia wa Ukraine, ninaweza kuwaambia nchi zote za Kisovieti kuwa watuangalie sisi, Kila kitu kinawezekana."
"Kama kura ziko sawa, basi atakuwa amechaguliwa kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano." Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa baadaye.
Zelensky anajulikana kwa umahiri wa ucheshi wake kama muigizaji nyota wa mfululizo wa filamu za ‘satirical’ katika televisheni ambapo anaigiza kama rais wa Ukraine.
Volodymyr Zelensky ni nani?
Zelensky amekuwa akicheza michezo ya kuigiza inayoitwa 'Servant of the People ' ambapo kwa bahati tu akawa muigizaji anayetaka kuwa rais wa Ukraine.
Anacheza kama mwalimu aliyechaguliwa baaada ya kufukuzwa kwa kosa la rushwa na kusambaa katika mitando ya kijamii.
Akiwa hana uzoefu wowote wa siasa, kampeni za Zelensky ziliangazia utofauti wake na wagombea wengine badala ya mawazo ya sera.