Marekani, Umoja wa Ulaya kusaini mkataba wa kimataifa matumizi ya AI

Muktasari:
- Lengo la Mkataba wa akili mnemba unazingatia zaidi ulinzi wa haki za binadamu za watu walioathiriwa na mifumo ya akili mnemba na ni tofauti na sheria ya Umoja wa Ulaya.
Uingereza. Mkataba wa kwanza wa kisheria wa kimataifa wa akili mnemba (AI) unatarajiwa kutiwa saini leo Alhamisi Septemba 5, 2024, baada ya majadiliano kati ya nchi 57.
Shirika la Haki za Binadamu la Baraza la Ulaya limesema mkataba huo utafunguliwa na kutiwa saini na nchi ambazo zilijadiliana, wakiwemo wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) na Marekani.
Sheria ya akili mnemba ya Umoja wa Ulaya inajumuisha kanuni za kina kuhusu uundaji, uwekaji na matumizi ya mifumo ya akili mnemba ndani ya soko la Umoja wa Ulaya.
Waziri wa Sheria wa Uingereza, Shabana Mahmood amesema mkataba huo ni hatua muhimu katika kuhakikisha teknolojia hizi mpya zinaweza kutumika bila kuharibu maadili, haki za binadamu na utawala wa sheria.
Mkataba wa akili mnemba unazingatia zaidi ulinzi wa haki za binadamu za watu walioathiriwa na mifumo ya akili mnemba inakinzana na sheria ya Umoja wa Ulaya, ambayo ilianza kutumika mwezi uliopita.
Ili kufikia malengo hayo, watafiti wa akili mnemba wamejadili njia mbalimbali za kutatua matatizo, zikiwemo za uboreshaji na utafutaji.
Serikali ya Uingereza imesema itafanya kazi na wadhibiti, tawala zilizogatuliwa na serikali za mitaa ili kuhakikisha inaweza kutekeleza mahitaji yake mapya ipasavyo.
Watia saini wanaweza kuchagua kupitisha au kuboresha hatua za kisheria za kiutawala au zingine ili kutekeleza masharti.
Kamati ya dharura ilianza uchunguzu mwaka 2019 na Kamati ya Ushauri iliundwa 2022 ambayo majukumu yake ilikuwa kutayarisha na kujadili kwa maandishi.
Imeandaliwa na Victoria Michaelkwa msaada wa mtandao.