Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Akili bandia yatumika kudanganya uwepo wa Rihanna 'Met Gala'

Muktasari:

  • Picha nyingine za mastaa ambao zimetengenezwa kwa kutumia AI (Akili Bandia) na Katy Perry, na Lady Gaga.

Baada ya kuripotiwa kuwa mwanamuziki Rihanna hakuweza kuhudhuria katika tamasha la mitindo la ‘Met Gala’ lililofanyika nchini Marekani, baadhi ya watu wametengeneza picha ‘feki’ za msanii huyo kwa kutumia AI (Akili Bandia) wakidai kuwa Riri alikuwepo katika maonyesho hayo.


                      

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini Marekani vimethibitisha kuwa mwanamuziki huyo hakuwepo katika maonesho hayo huku wakiwataka mashabiki wa mataifa mengine kupuuzia uvumi huo.

Hata hivyo, kupitia ukurasa wa Instagram wa Katy Perry ame-share picha hiyo iliyotengenezwa na AI na kukanusha kuwa mwanamuziki huyo hakuwepo kwenye ‘Met Gala’ kutokana na kuwa na kazi nyingi.

Picha nyingine za mastaa ambao zimetengenezwa kwa kutumia AI (Akili Bandia) na Katy Perry, na Lady Gaga.


                     

Ikumbukwe kuwa tovuti ya People ilidai kuwa ilimtafuta mmoja wa watu wa karibu wa Riri ambapo alidai kuwa mwanamuziki huyo aliamua kughairi kuhudhuria tamasha hilo kutokana na kuumwa na mafua.