Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo makubwa matano yaliyojiri maandamano ya Gen-Z Kenya

Muktasari:

  • Vifo, vurugu na uporaji ni miongoni mwa mambo yaliyojitokeza Jumatano Juni 25, 2025 kwenye maandamano ya Gen-Z nchini Kenya.

Dar es Salaam. Jumatano ya Juni 25, 2025 yalifanyika maandamano ya raia, , wengi wao wakiwa vijana maarufu Gen-Z, katika majiji ya Nairobi, Mombasa na miji mingine nchini Kenya, lengo likiwa ni kuadhimisha mwaka mmoja tangu wenzao wauawe kwenye maandamnao yaliyofanyika mwaka 2024.

Kwa mujibu wa vyombo vya nchini humo, takriban watu 60 waliuawa na vikosi vya usalama mwaka jana, katika wiki za maandamano ya kupinga ongezeko la ushuru na hali mbaya ya kiuchumi kwa vijana wa Kenya.

Kufuatia hilo Gen-Z walipanga kufanya maandamano ya maadhimisho, ambayo awali asubuhi yalikuwa ya amani ingawa muda ulivyozidi, vurugu na hekaheka zikaibuka na risasi na mabomu ya machozi yakarindima.


Mambo matano yaliyojiri

Jambo la kwanza lililojitokeza ni tamko la Serikali kuwa waandamanaji walijaribu kupindua Serikali ya nchi hiyo.

Akinukuliwa na BBC, Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen alisema maandamano hayo yalichochewa na baadhi ya wanasiasa wanaotumia vijana vibaya, wakiwa na lengo la kuipindua Serikali.

Jambo la pili ni watu mashuhuri kujitokeza kwenye maandamano, wakiwemo wanasiasa na wasanii, baadhi yao ni Jaji Mkuu mstaafu, David Maraga na Eugene Wamalwa, mbunge wa Embakasa Mashariki, Kalonzo Musyoka na Babu Owino walionekana barabarani wakiungana na vijana waliokuwa wakiimba nyimbo za kutaka haki.

Wasanii wa muziki wakiwemo, Arrow Bwoy na Khaligraph Jones, nao walijitokeza kushiriki maandamano hayo ambayo kwa upande mwingine yalipinga ukatili wa polisi na kudai haki ya raia.

Jambo la tatu, bunduki tano ziliibwa, vituo vinne vya polisi vilichomwa moto. Hii ni ilibainika baada ya Waziri Murkomen kuzuru maeneo husika.

Kama haitoshi, biashara zilivunjwa na mali za umma kuharibiwa na Murkomen alilaani kile alichokitaja kuwa kampeni ya vurugu iliyopangwa na iliyojificha chini ya kivuli cha maandamano ya amani.

"Vituo kadhaa vya polisi vilishambuliwa na bunduki kuibiwa, mali zimeporwa na kuharibiwa, barabara kuchafuliwa, vituo vya polisi tisa vilivamiwa, kati ya hivyo, vitano, vikiwemo Dagoretti, Molo na Ol Kalou vimechomwa moto" Morkomen alinukuliwa na Tuko News ya Kenya.

Aliongeza: “Magari 88 ya polisi yameharibiwa, pamoja na magari 27 ya Serikali kutoka idara za kitaifa na kaunti. Zaidi ya magari 65 ya raia, yakiwemo mabasi ya shule yaliyokuwa yameegeshwa katika vituo vya polisi yalichomwa moto,” alisema.

Jambo la nne vifo vya watu 16 na majeruhi. Katika siku hiyo watu 16 wameripotiwa kuuawa kwa mujibu wa BBC, huku zaidi ya 400 wakjeruhiwa wakiwemo maofisa 300 wa polisi.

Kwa mujibu wa Shirika la haki za kibinadamu, Amnesty International, chanzo cha vifo hivyo ni majeraha ya risasi.

Mkurugenzi mkuu wa Amnesty International, Irungu Houghton amesema idadi hiyo imethibitishwa na tume ya kitaifa ya haki za kibinadamu nchini Kenya.

Jambo la tano ni vyombo vya habari kuzuiwa kurusha matangazo mubashara ya maandamanyo hayo. Siku hiyo, kupitia taarifa ya Tume ya Mawasiliano Kenya (CAK), ikiwa ni saa chache tangu waandamanaji waingie mtaani, vyombo vya habari vilipigwa marufuku kurusha matangazo.

Serikali iliamuru vyombo vyote vya habari vinavyoendesha televisheni na redio Kenya kusitisha urushaji wa matangazo ya moja kwa moja ya maandamano.

Mkurugenzi Mkuu wa CAK, David Mugonyi, kupitia taarifa hiyo, alisema matangazo ya moja kwa moja ya maandamano yanakiuka kifungu cha 33 (2) na 34 (1) cha Katiba ya Kenya pamoja na Sehemu ya 461 ya Sheria ya Mawasiliano na Habari ya Kenya ya mwaka 1998.