Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kusambaa mashambulizi ya Iran kwazua hofu Mashariki ya Kati

Muktasari:

  • Tukio kubwa zaidi limeripotiwa nchini Jordan ambako mashambulizi yalilenga Kambi ya Anga ya Muwaffaq Salti, maarufu kama Kituo cha Anga cha Azraq, kinachotumiwa na Jeshi la Anga la Jordan huku pia kikihudumia shughuli za ushirikiano wa kijeshi kati ya Jordan na Marekani.

Dar es Salaam. Iran imeongeza mashambulizi yake katika Mashariki ya Kati baada ya kuripotiwa kulenga Jordan, Bahrain, Kuwait na Qatar, hatua inayozidisha mvutano kati yake na Marekani pamoja na washirika wake na kuongeza hofu ya mzozo huo kugeuka vita vya kikanda.

Tukio kubwa zaidi limeripotiwa nchini Jordan ambako mashambulizi yalilenga Kambi ya Anga ya Muwaffaq Salti, maarufu kama Kituo cha Anga cha Azraq, kinachotumiwa na Jeshi la Anga la Jordan huku pia kikihudumia shughuli za ushirikiano wa kijeshi kati ya Jordan na Marekani.

Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani katika Mashariki ya Kati (CENTCOM) ilithibitisha kuwa wanajeshi wawili wa Marekani waliuawa na mwingine kutoweka wakati vikosi vya Marekani na washirika wake vikijibu mashambulizi ya Iran kwa makombora ya balistiki na ndege zisizo na rubani.

Katika taarifa yake ya Julai 18, 2026, CENTCOM ilisema, "Wanajeshi wawili wa Marekani nchini Jordan waliuawa vitani wakati Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani na vikosi washirika vikijilinda dhidi ya mashambulizi ya Iran kwa makombora ya balistiki na ndege zisizo na rubani. Aidha, mwanajeshi mmoja bado hajulikani aliko," ilisema taarifa hiyo.

Kwa upande wake, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) la Iran limetangaza kuwa lilifanya mashambulizi kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya maeneo lililodai yalikuwa yakitumika na vikosi vya Marekani katika eneo hilo, likieleza hatua hiyo ni sehemu ya operesheni zake za kijeshi dhidi ya Marekani na washirika wake.

Mashambulizi hayo yameongeza taharuki mataifa ya Bahrain, Kuwait na Qatar ambako pia kuna vituo vya kijeshi vya Marekani na miundombinu muhimu ya ulinzi.

 Nchi hizo zimeimarisha zinaripokuwa kuwa zimeimarisha tahadhali za kiusalama huku zikifuatilia kwa karibu mwenendo wa mapigano.


Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imelaani mashambulizi hayo katika taarifa yake ya Julai 21, 2026 ikisema, mashambulizi mapya ya Iran dhidi ya Jordan, Bahrain na Kuwait yanahatarisha usalama na utulivu wa Mashariki ya Kati.

Aidha, kuongezeka kwa mashambulizi hayo pia kumeongeza wasiwasi kuhusu usalama wa Mlango wa Hormuz, njia muhimu inayopitisha sehemu kubwa ya mafuta yanayosafirishwa duniani.

 Wataalamu Katika ukanda huo, wanaonya kuwa mzozo ukiongezeka unaweza kuendelea kuvuruga usafirishaji wa mafuta, kuongeza gharama za bima za meli na kusababisha kupanda zaidi kwa bei ya nishati katika soko la dunia.

Kwa wananchi wa eneo hilo, hali ya kiusalama imeendelea kuwa ya hofu kutokana na kuimarishwa kwa ulinzi katika vituo vya kijeshi, viwanja vya ndege na miundombinu muhimu, huku serikali mbalimbali zikichukua hatua za tahadhari dhidi ya mashambulizi mengine yanayoweza kutokea.

Wakati mapigano yakiendelea, macho ya dunia yanaendelea kuelekezwa Mashariki ya Kati huku hofu ikiongezeka kwamba mashambulizi yanayozifikia Jordan, Bahrain, Kuwait na Qatar yanaweza kuufanya mzozo kati ya Iran na Marekani kuingia katika hatua mpya ya kuenea Mashariki ya Kati na kuvuruga uchumi wa dunia.

Hatua hiyo inaendela huku Umoja wa Mataifa (UN) ukitoa wito kwa raia waliokwama katika mlango wa Hormuz kuokolewa na kuachiwa huru.