Konda aua abiria, daladala yachomwa moto

Muktasari:

  • Wananchi wenye hasira kali wamechoma moto daladala ambayo konda alimrusha nje wakati ikiwa inatembea abiria aliyepungukiwa nauli na kumsababishia umauti.

Kenya. Ukisoma kichwa cha habari unaweza ukashtuka lakini ndio ukweli kwamba konda amekatisha uhai wa abiria wake aliyepungukiwa nauli huko nchini Kenya.

Tukio hilo limetokea jana Jumatano Mei 17 katika Barabara ya Outering iliyoko jijini Nairobi, ambapo mzozo uliibuka kati ya konda na abiria huyo mwenye umri wa miaka 17 aliyepungukiwa kiasi cha nauli cha KSh 20.

Inadaiwa mabishano yalizidi kati ya konda na abiria huyo hivyo konda akaamua kumtupa nje wakati gari hilo likiwa kwenye mwendo, kwa bahati mbaya gari hilohilo ndilo lililomkanyaga na kumuuwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tuko ya nchini humo imesema konda huyo alichanja mbuga baada ya wakazi na wapita njia wa eneo hilo kuamua kulichoma moto gari hilo.