Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Iran yashambulia hospitali Israel, yenyewe yalipua mtambo wa nyuklia

Tel Aviv. Kombora lililorushwa kutoka Iran limelenga jengo la hospitali kuu iliyopo kusini mwa Israel na kusababisha majeruhi kadhaa, huku yenyewe ikijibu kwa kushambulia mtambo wa urutubishaji nyuklia.

Mamlaka nchini humo zimethibitisha kuwa Iran imefanya shambulio hilo asubuhi ya leo Alhamisi Juni 19, 2025, huku taarifa zikisema bado tathmini ya madhara zaidi yaliyosababishwa na kombora hilo inaendelea.

Ofisa kutoka Idara ya Dharura ya Israel, Magen David Adom ameieleza Associated Press kuwa makombora mengine ya Iran yalipiga kwenye majengo mawili jijini Tel Aviv nchini humo na kujeruhi watu 40.

Kombora hilo lilitua Kituo cha Matibabu cha Soroka, ambacho huwadumia wagonjwa wengi Kusini mwa Israel.

Taarifa ya hospitali hiyo ilisema kuwa sehemu kadhaa za jengo hilo ziliharibiwa na kwamba kuna majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu.

Hospitali hiyo ilifungwa kwa muda ili kuzuia wagonjwa kuingia isipokuwa kwa wale walioko kwenye hali mbaya. Haikufahamika mara moja idadi ya watu waliojeruhiwa katika shambulio hilo.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amelaani shambulio hilo na kuahidi kulipiza kisasi, akisema: “Madikteta wa Iran wataadhibiwa kulingana na gharama za matendo yao.”

Hospitali nyingi nchini Israel zimekuwa katika mipango ya dharura  tangu wiki iliyopita, ikiwemo kubadili sehemu za maegesho ya magari kuwa wodi na kuwahamisha wagonjwa chini ya ardhi (under ground floor), hasa wale waliowekewa mashine za kusaidia kupumua.


Mtambo wa nyuklia walengwa

Israel nayo imefanya mashambulizi ikiulenga mtambo wa urutubishaji  nyuklia wa Arak, tukio linalotajwa kuwa shambulio hatari zaidi  nchini humo ikiwa ni siku ya saba tangu kuanza kwa mvutano baina ya mataifa hayo.

Hata hivyo, mamlaka nchini Iran zimetoa taarifa zikisema hakuna hatari ya kiafya iliyosababishwa na mtambo huo baada ya kulipuliwa.

Iran imefyatua makombora mfululizo na kurusha ndege zisizo na rubani, ingawa makombora mengi kati ya hayo yamedunguliwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel.

Hata hivyo, Associated Press imeripoti kuwa maofisa nchini Israel wanakiri kuwa mfumo wao umeanza kutetereka kiasi cha kuruhusu makombora ya IIran kupenya na kusababisha madhara kwa raia.

Jeshi la Israel limesema ndege zake za kivita zililenga mtambo wa Arak na muhuri wa sehemu ya ndani ya mtambo huo ili kuharibu uzalishaji wa plutoniamu.

Taarifa ya jeshi ilisema: “Shambulio lililenga sehemu ya uzalishaji wa plutoniamu ili kuzuia  maendeleo ya uzalishaji silaha za nyuklia.”

Baada ya taarifa hiyo ya Iran, Israel imeibuka na kudai kuwa imelenga eneo jingine karibu na Natanz linalohusiana na mpango wa urutubishaji nyuklia.

Televisheni ya taifa ya Iran imeripoti kuwa: “Hakuna hatari ya mionzi kutokana na shambulio hilo la Arak.”

Kwa mujibu wa televisheni ya taifa ya Iran, imesema tahadhari ilikuwa imeshachukuliwa kabla ya kutokea shambulizi hilo ambapo wafanyakazi wote walikuwa wamehamishwa kutoka eneo hilo.

Mashambulizi hayo yamefanyika ikiwa ni siku moja baada ya Kiongozi Mkuu wa Iran kukataa wito wa Marekani wa kujisalimisha na kuonya kuwa ushiriki wowote wa kijeshi wa Marekani utaufanya mgogoro huo kuwa vita kamili.

Kampeni ya Israel imelenga maeneo ya kurutubisha urani ya Iran huko Natanz na mtambo wa nyuklia wa Isfahan. Mashambulizi hayo yanayoendelea ya Israel pia yamewaua majenerali wa ngazi ya juu na wanasayansi wa nyuklia.

Kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za binadamu wa Iran wenye makao makuu yao Washington, watu wasiopungua 639, wanajeshi 376 na raia raia 263, wameuawa nchini Iran na zaidi ya 1,300 wamejeruhiwa.

Katika kulipiza kisasi, Iran imefyatua takriban makombora 400 kwa kutumia ndege zisizo na rubani na kuua takriban watu 24 nchini Israel huku mamia wakijeruhiwa.


Imeandikwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa Mashirika ya Habari.