Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Idadi ya vifo vya tetemeko la ardhi Afghanistan vyafikia 2,000

Muktasari:

  • Idadi ya vifo kutokana na matetemeko ya ardhi yaliyotokea Magharibi mwa Afghanistan imeongezeka hadi kufikia zaidi ya watu 2,000, maelfu wamejeruhiwa huku waokoaji wakitafuta wengine walionasa.

Herat. Idadi ya vifo kutokana na matetemeko ya ardhi yaliyotokea Magharibi mwa Afghanistan imeongezeka hadi kufikia zaidi ya watu 2,000 huku maelfu wakiwa wamejeruhiwa.

Jana Jumamosi Oktoba 8, 2023 tetemeko lenye ukubwa wa 6.3 lilitikisa nchi hiyo huku likifuatiwa na mengine nane Kaskazini-Magharibi mwa Mji Mkuu wa Mkoa wa Herat, ambapo ziliangushwa nyumba na kuwafanya wakazi kukimbia.

Shirika la Habari la AFP limesema Serikali ya Taliban imetoa taarifa yake leo Jumapili kwamba ni mfululizo wa matetemeko mabaya zaidi kuikumba nchi hiyo katika miaka mingi ambayo yamesababisha maafa.

"Watu 2,053 wamefariki katika vijiji 13 huku wengine 1,240 wakijeruhiwa. Nyumba 1,320 zimeharibiwa kabisa," Msemaji wa Serikali ya Taliban Zabihullah Mujahid, ameandika kwenye mtandao wa X.

Habari zaidi zinasema katika Jiji la Herat, wakati tetemeko la kwanza linatokea kulikuwa na ripoti chache za vifo na majeruhi lakini baadaye iliwalazimu raia kuzikimbia nyumba zao.

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, limesema idadi ya majeruhi inatarajiwa kuongezeka huku shughuli za utafutaji na uokoaji zikiendelea.

Ikumbukwe mwaka huu kumekuwa na matukio ya matetemeko ya ardhi yaliyozikumba nchi mbalimbali Kaskazni mwa Afrika na barani Asia ikiwemo tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria lililoua takriban watu 50,000 mapema Februari na jingine nchini Morocco.