Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gen ‘Z’ waliamsha tena Kenya, shule zafungwa Nairobi

Muktasari:

  • Japo haijafahamika lengo la vijana nchini humo kuingia barabarani hata hivyo, taarifa zinadai azma ya vijana hao ni kupinga hali ya maisha inayoendelea pamoja na kutoridhishwa na utendaji kazi Serikali nchini humo likiwamo Bunge.

Nairobi. Kenya bado hakujatulia. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya maelfu ya vijana nchini humo kuingia barabarani wakiandamana.

Japo haijafahamika lengo la vijana nchini humo kuingia barabarani hata hivyo, taarifa zinadai azma ya vijana hao ni kukumbuka mauaji ya wenzao katika maandamano ya mwaka 2024, kupinga hali ngumu ya maisha inayoendelea pamoja na kutoridhishwa na utendaji kazi Serikali nchini humo likiwamo Bunge.

Tovuti ya Dail Nation ya nchini humo, imeripoti leo Jumatano Juni 25, 2025, kuwa katika Jiji la Nairobi ambako mkutano wa Bunge ulipangwa kuendelea leo Jumatano Juni 25, 2025, maofisa usalama walilazimika kuweka kizuizi ili kuhakikisha hawafiki kwenye viunga vya Bunge hilo.
Pia, imeripoti kuwa shule zimefungwa kwa hofu ya kuepuka maafa kutokana na maandamano hayo.

Mwaka jana vijana waliandama nchini humo kupinga muswada wa fedha na ongezeko la kodi jambo lililomlazimu Rais William Ruto kufanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri.

Hata hivyo, hadi Rais Ruto anachukua uamuzi huo wa kubadilisha baraza la mawaziri, Serikali nchini humo iliripoti waandamanaji zaidi ya 60 kuuawa katika maandamano na makabiliano dhidi ya vikosi vya ulinzi na usalama nchini humo.

Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi na vilipuzi kuzuia maandamano hayo ambayo hadi kufikia Saa 7:00 mchana yalikuwa yamesambaa katika Kaunti 12 nchini humo.

Bado haifahamika madhara ambayo yamejitokeza upande wa polisi ambao wako kwenye mzozo mkubwa na waandamanaji ambao wengine wamejimahi kwa silaha za jadi.

Jaji Mkuu mstaafu wa Kenya, David Maraga, mwanasiasa na kiongozi wa upinzani nchini humo, Kalonzo Musyoka na Eugene Wamalwa ni miongoni mwa watu walioonekana barabarani wakiungana na vijana hao.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya, imechapisha kwenye akaunti yake ya mtandao wa X, ikiwataka wananchi kutii sheria. “Heshimuni sheria, kila mtu awajibike kwa nafasi yake,” imeandika.

Endelea kufuatilia Mwananchi…..