Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgodi wa dhahabu Magambazi kuanza rasmi Julai

Muktasari:

  • Mgodi wa Madini ya dhahabu wa Magambazi uligunduliwa na wachimbaji wadogo mnamo mwaka 2003 ambapo baadae waliondolewa na kupewa kampuni ya Canaco Tanzania Ltd,ikaingia kampuni ya Tanzania Gold Field na sasa ipo Kampuni ya PMM Tanzania Limited,ila mpaka sasa serikali imedai kutoridhishwa na utendaji kazi wao.

Handeni. Wizara ya Madini imeridhia Kampuni za PMM Tanzania Limited na East African Metals (CANACO) watafute mwekezaji mwingine wa tatu mwenye nguvu  ili kuendesha mgodi wa Dhahabu wa Magambazi uliopo wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,ambao umekuwa ukisuasua kufanyakazi kwa muda mrefu.

Waziri wa Madini Anthony Mavunde ameeleza hayo wakati akitoa muafaka ambapo alitoa siku 30 kwa kampuni hizo, kuangalia ni jinsi gani wataweza kufanyakazi ambapo serikali itapata masrahi   leo Jumamosi  Mei 10, 2025, wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nyasa, na kutoa  agizo hadi  Julai Mosi kazi zianze.

Waziri Mavunde, ameeleza kuwa Mgodi wa Kati wa Dhahabu wa Magambazi kwa makubaliano waliowekeana na wawekezaji utaanza kufanya kazi rasmi ifikapo Julai Mosi,2025 na mwekezaji wa tatu atatangazwa na Serikali baada ya kuripoti ofisini kwake kuona kama atakuwa amekidhi vigezo.

Amesema kufanikiwa kwa utaratibu huo unatarajiwa kuleta tija kwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Kijiji cha Nyasa na Wilaya ya Handeni kwa ujumla, kwani tangu kuanza migogoro ya kiutendaji hata wananchi wameathirika kwa kukosa ajira katika eneo hilo.

"Huyo mtu atateuliwa ndani ya siku 14 kuanzia Jumatatu ya Mei 12,2015 mpaka Mei 26, litatolewa jibu ni nani kutoka nchi gani atakuwa wa tatu katika kuendesha mgodi huu wa Magambazi ambae yeye atafanyakazi zote za kiufundi na kuleta wataalam wa kisasa ikiwemo mashine ambapo kazi rasmi itaanza Julai Mosi 2025," amesema Waziri Mavunde.

Amesema baada ya kuchukua hatua ya kupata mwafaka wa kuhakikisha mgodi huo unaanza kufanya kazi, kampuni nyingine ya tatu itateuliwa ambapo itaungana na kampuni za PMM na East African Metals/CANACO ili kuendesha mgodi huo.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Handeni, Albert Msando ambaye amehamishiwa Wilaya ya Ubungo kwa  sasa amesema ameshakubaliana na wawekezaji pamoja na wananchi kuhusu kugawana asilimia ya mauzo yatakayopatikana na wamekubali kufanya hivyo kwa pande zote zinazohusika.

Msando amesema katika makubaliano hayo wale wenye asilimia 85 wameridhia zimepunguzwa na kupewa wenzao wengine, ambapo wamekubali na kuondoa tofauti zao na mwekezaji anaekuja atasimamia makubaliank hayo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya PMM Tanzania Limited Spendi Ulimbakise amesema makubaliano hayo yatakuwa na tija endapo uzalishaji utaanza,kwani wataweza kuajiriwa zaidi ya wananchi 300 ukiacha vibarua.

Amesema eneo hilo la Magambazi kuna dhahabu nyingi hivyo ukifanyika uwekezaji mzuri utasaidia kuzalishwa dhahabu nyingi itakayosababisha hata mapato ya wilaya na wananchi wa Handeni kuongezeka.

Mbunge wa Handeni Vijijini, John Sallu amesema Serikali imekuwa ikikosa mapato kutokana na kuendelea mgogoro huo,hivyo endapo Serikali itasaidia kupatikana kwa mwekezaji wa tatu itakuwa ni  motisha kwa wale waliopo.

Kampuni inayotafutwa sasa itakuwa ya nne katika mgodi huo wa dhahabu wa Magambazi ambapo imetanguliwa na kampuni ya  Canaco Tanzania Ltd,Tanzania Gold Field na Kampuni ya PMM Tanzania Limited ambazo uzalishaji wake kwa maelezo ya serikali hauridhishi.