Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi kupata huduma za madini mahali pamoja

Muktasari:

  • Wizara ya Madini imeondoa usumbufu wa wananchi kusafiri maeneo mbalimbali kutafuta huduma baada ya kumalizika kwa jengo la makao makuu ya wizara hiyo lililopo Mtumba, jijini Dodoma. Jengo hili linatoa fursa kwa wananchi kupata huduma zote muhimu kwa urahisi na karibu.

Dodoma. Changamoto ya wananchi kusumbuka kuzunguka maeneo mbalimbali kutafuta huduma za Wizara ya Madini imekwisha, baada ya wizara hiyo kukamilisha ujenzi wa jengo la makao makuu lililopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, na kuhamia rasmi.

Kuhamia katika jengo hilo ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, Machi 20, 2025, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea ujenzi wa jengo hilo.

Mavunde amesema lengo kuu la hatua hiyo ni kurahisisha utoaji wa huduma bora na za haraka kwa wananchi.

Akizungumza leo Mei 15, 2025 wakati akiingia kwa mara ya kwanza katika jengo hilo, Mavunde amesema Watanzania wote watahudumiwa kupitia jengo hili na kuondoa usumbufu wa kuzunguka katika ofisi tofauti kutafuta huduma.

“Hapo awali kulikuwa na changamoto kubwa kutokana na ufinyu wa ofisi, Mtanzania akija hapa kupata huduma alikuwa akilazimika kwenda katika ofisi nyingine zilizopo mjini kwa sababu vitengo vyote havikuwepo katika eneo moja,” amesema.

Amesema uamuzi wa kuhamia Mtumba utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi kwa kuwaondolea usumbufu wa kuwatafuta wataalamu katika maeneo mbalimbali, huku pia ukiwa ni njia ya kuokoa muda wao na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Mavunde amesema kuwa ujenzi wa jengo la Tume ya Madini uko katika hatua za mwisho na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni, ambapo mara tu litakapokamilika, tume hiyo itahamia rasmi katika jengo hilo lililopo Mtumba, jijini Dodoma.

Hatua hiyo itahitimisha mchakato wa taasisi zote za wizara kuhamia Mji wa Serikali, isipokuwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ambayo itaendelea kubaki mjini kwa sababu maalumu za kiutendaji.

Naye Naibu Waziri wa Madini, Steven Kiruswa ametaka watumishi kuongeza ufanisi wa kazi zao baada ya kupata ofisi hizo kwa kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya mazingira ya kufanya kazi na matokeo ya kazi.

“Ukiangalia kila mtu ana nafasi nzuri ya kufanya kazi katika jengo hili ambayo inaweza kumfanya asitamani kutoka anapoingia. Hili jengo ni zuri sana,” amesema.

Mkandarasi wa jengo hilo ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na linajengwa kwa gharama ya Sh22.8 bilioni na mshauri elekezi ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Jengo hilo ni sehemu ya awamu ya pili ya ujenzi huo ilizinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Desemba 2 mwaka 2021 ambapo unahusisha ujenzi wa ofisi za wizara 23 na utagharimu Sh300 bilioni.

Awamu ya kwanza ya ujenzi wa ofisi hizo ulianza Novemba 28 mwaka 2018 na kukamilika Machi 22 mwaka 2019 ambapo jumla ya Sh39.38 bilioni zilitumika.