Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wataka mbinu mpya usimamizi wa fedha

Muktasari:

  • Wadau wamesema kutumiwa kwa mbinu mpya za usimamizi wa fedha kutaimarisha shughuli hiyo Afrika Mashariki.

Dar es Salaam. Wataalamu wa usimamizi wa fedha, wamesema ni muhimu kuwepo ubunifu, mageuzi ya kimkakati na uundaji wa thamani ya muda mrefu katika usimamizi wa fedha, badala ya kutumia mbinu za jadi.

Wamesema kufanya hivyo, kutaimarisha shughuli ya usimamizi wa fedha nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla wake.

Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Obedi Laiser katika mkutano wa 10 wa maofisa wakuu wa fedha (CFO), uliohudhuriwa na wataalamu zaidi 100 kutoka Afrika Mashariki.

Amesema hatua yao ya kudhamini mkutano huo ni mwendelezo wa dhamira yao ya kuendeleza Afrika kwa kusaidia taasisi na viongozi wake wa kifedha.

“Tunatambua nafasi nyeti ya viongozi wa fedha katika kusuka mustakabali wa taasisi mbalimbali Afrika Mashariki. Nafasi ya CFO imepanuka zaidi ya usimamizi wa kifedha wa jadi, sasa inahusisha ubunifu, mageuzi ya kimkakati na uundaji wa thamani ya muda mrefu,” amesema Laiser.

Amesema wataendelea kutoa suluhisho mahususi la kifedha na ushauri wa kimkakati ili kusaidia taasisi mbalimbali kustawi katika mazingira ya kiuchumi yenye changamoto nyingi.

“Tupo tayari kushirikiana na maofisa wa fedha kwa kuwapatia maarifa, mitaji na utaalamu utakaowasaidia kufanikisha malengo yao na kufungua fursa mpya za ukuaji,” amesema.

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika mkutano huo ni mabadiliko ya nafasi ya CFO, mageuzi ya kidijitali, ujumuishaji wa masuala ya mazingira, jamii na utawala bora na mbinu bora za ukuaji wa kimkakati na usimamizi wa mitaji.

Kwa mujibu wa waandaaji, mkutano huo ulikuwa jukwaa la wataalamu wa fedha kuandaa mbinu za kukabiliana na changamoto zinazoikumba sekta hiyo, sambamba na kuimarisha mwelekeo wa ukuaji endelevu wa biashara katika ukanda huu wa Afrika.

Ushiriki wa Absa Tanzania unaenda sambamba na kauli mbiu yake ya “Stori yako ina thamani” kuwawezesha Waafrika kupitia ushirikiano wa kimkakati, ubunifu na uongozi wa fikra.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja wa Mashirika wa benki hiyo, Nellyana Mmanyi amesema benki hiyo ina uwezo mpana wa kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja kwa wakati husika.

“Huduma zetu zinaanzia katika ushauri wa kifedha, ufadhili wa miradi na mali, hadi katika masoko ya mitaji. Tunachokitoa si bidhaa tu, bali ni ushirikiano wa kimkakati unaozingatia hali halisi ya kufanya biashara Tanzania na Afrika kwa ujumla,” amesema.