Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vipaumbele tofauti bajeti za Afrika Mashariki zikiongezeka

Muktasari:

  • Mwenendo wa bajeti hizo unaonesha kuongezeka mwaka hadi mwaka, huku Kenya ikiwa na bajeti kubwa kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki, ikifuatiwa na Tanzania, Uganda na Rwanda

Dar es Salaam. Mawaziri wa Fedha wa Afrika Mashariki wamewasilisha bajeti kuu za Serikali zao kwa mwaka wa fedha 2025/26, huku wakikabiliwa na mazingira magumu ya kiuchumi pamoja na mizozo ya kisiasa duniani na katika kanda.

Nchi zilizowasilisha bajeti zao leo Juni 12, 2025 ni Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda zinazonesha tofauti katika vipaumbele huku zikiweka mkazo kwenye vyanzo vipya vya mapato.

Mwenendo wa bajeti hizo unaonesha kuongezeka mwaka hadi mwaka, huku Kenya ikiwa na bajeti kubwa kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki, ikifuatiwa na Tanzania, Uganda na Rwanda.


Bajeti ya Kenya

Waziri wa Fedha wa Kenya, John Mbadi amewasilisha bajeti ya Dola 33.03 bilioni za Marekani (Sh85.382 trilioni) kwa mwaka wa fedha 2025/26, ikiwaka mkazo zaidi katika hatua za kuongeza mapato ya Serikali.

Waziri wa Fedha wa Kenya, John Mbadi

Serikali ya Kenya inakadiria kukusanya Dola 25.63 bilioni (Sh66.1 trilioni) ya mapato ya kawaida na fedha za matumizi maalumu, huku Dola 7.06 bilioni (Sh18.2 trilioni) zikipatikana kupitia mikopo ya ndani na nje ya nchi.

Wakati mpango wa bajeti ukiwasilishwa bungeni, polisi waliwatawanya waandamanaji katikati ya Jiji la Nairobi kwa kutumia gesi ya kutoa machozi wakati wa maandamano baada ya kifo tata cha mwalimu na mwanablogu, Albert Ojwang.

Maandamano hayo yaligeuka vurugu baada ya baadhi ya waandamanaji kuchoma magari mawili eneo la Aga Khan Walk, karibu na jengo la Uchumi House na kuharibu mali, jambo lililosababisha biashara zilizo karibu kufungwa.


Bajeti ya Tanzania

Bajeti ya Tanzania ya mwaka 2025/26, iliyowasilishwa na Serikali ni ya Sh56.49 trilioni (Dola 21.6 trilioni) zinazotarajiwa kukusanywa na kutumika katika mwaka 2025/26. Bajeti hii inatarajiwa kugharamiwa na mapato ya ndani ya Sh40.47 trilioni, misaada Sh1.07 trilioni na mikopo ya Sh14.95 trilioni.

Akiwasilisha bajeti hiyo, Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba amesema kati ya mapato ya ndani yanayotarajiwa, mapato ya kodi ni Sh32.31 trilioni, mapato yasiyo ya kodi ni Sh6.48 trilioni na mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ni Sh1.68 trilioni.

Pia , amesema mikopo inajumuisha Sh6.27 trilioni kutoka vyanzo vya ndani na Sh8.68 trilioni kutoka vyanzo vya nje.

Makadirio ya matumizi ya Serikali ya Sh56.49 trilioni kwa mwaka 2025/26 yanajumuisha: stahiki za watumishi na michango ya pensheni (Serikali Kuu) Sh9.17 trilioni; ununuzi wa bidhaa na huduma Sh5.58 trilioni; malipo ya riba za mikopo Sh6.49 trilioni; na ruzuku kwa taasisi za Serikali, mashirika ya umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa Sh22.17 trilioni.

Pia, Serikali inatarajia kutumia Sh7.72 trilioni kugharamia malipo ya mtaji kwa deni la ndani na nje.


Bajeti ya Uganda

Waziri wa Fedha wa Uganda, Matia Kasaija amewasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26 iikiwa imeongezeka kwa asilimia 0.3 kutoka Ush72.1 trilioni katika mwaka wa fedha 2024/25 hadi kufikia Ush72.3 trilioni (Dola 20.1 bilioni).

Waziri wa Fedha wa Uganda, Matia Kasaija

Ongezeko hilo linatokana na msaada wa bajeti ulioongezeka kwa kiasi kidogo, kutoka Ush1.39 trilioni hadi Ush2.08 trilioni, sawa na ongezeko la karibu asilimia 50, pamoja na mikopo ya ndani inayotarajiwa kuongezeka kutoka Ush8.97 trilioni hadi Ush11.38 trilioni,  ongezeko la takriban asilimia 26.9.

Vipaumbele vya bajeti hiyo ni uwekezaji katika shughuli za mafuta na gesi na miradi ya miundombinu kama vile matengenezo ya barabara na madaraja, ukarabati wa reli ya njia ya kawaida (meter gauge railway), ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), pamoja na usafiri wa majini.


Bajeti la Rwanda

Nchini Rwanda, Waziri wa Fedha Yusuf Murangwa amewasilisha bajeti ya Dola 4.9 bilioni (Sh12.8 trilini) kwa mwaka wa fedha 2025/26, unaoanza Julai.

Waziri wa Fedha wa Rwanda, Yusuf Murangwa

Serikali ya Rwanda inatarajia kutumia Dola 840 milioni (Sh2.19 trilioni) sawa na ongezeko la asilimia 21 ikilinganishwa na bajeti ya Rwf5.8 trilioni (Dola 4.06 bilioni) kwa mwaka wa sasa wa fedha.

Maeneo ya kipaumbele ni pamoja na ujenzi wa uwanja mpya wa ndege huko Bugesera, pamoja na sekta za kilimo, elimu, afya, makazi na uboreshaji wa upatikanaji wa umeme.

Serikali inatarajia kukusanya Dola 2.87 bilioni (Sh10.4 trilioni) kutokana na mapato ya ndani, ambayo ni sawa na asilimia 58 ya bajeti nzima.