Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yazuia ndege za Kenya Airways kutua Dar

Dar es Salaam. Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) imetangaza kusitisha kibali cha Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kufanya safari kati ya Jiji la Dar es Salaam na Nairobi kuanzia Januari 22, 2024.

TCAA inasema uamuzi huo unajibu hatua iliyochukuliwa na mamlaka za usimamizi wa anga la Kenya, kukataa maombi ya safari zote za ndege za mizigo zilizoombwa na Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) lililotaka kufanya safari kati ya Nairobi na mataifa mengine.

“Uamuzi uliofanyika ni kinyume cha kifungu namba nne cha mkataba wa ushirikiano wa huduma za anga kati ya Kenya na Tanzania ulioingiwa Novemba 24, 2016,” amesema Mkurugenzi wa TCAA Hamza Johari akielezea kuhusu kitendo kilichofanywa na mamlaka za usafiri wa anga za Kenya.

“Kufuatia uamuzi tulioufanya hakutakuwa na safari za ndege za abiria kwa shirika la ndege la KQ kati ya Dar es Salaam na Nairobi kuanzia Januari 22, 2024,” amesema Johari katika taarifa TCAA kwa umma iliyotolewa leo Januari 15, 2024.

Aidha TCAA imesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuheshimu mkataba wa Chicago wa mwaka 1944 na makubaliano ya ushirikiano katika anga kati yake na mataifa mengine.