Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tishio la usalama laichepusha KQ, yatua Stansted badala ya Heathrow

Muktasari:

  • Ndege hiyo KQ100, ilielekezwa kutua katika uwanja huo ambao ni mahsusi kwa utuaji salama kutokana na kile kilichodaiwa ni tishio la kiusalama, ambapo vyombo vya habari nchini humo, vimeripoti kuwa vikosi vya uteguaji mabomu vimeonekana kukimbilia eneo la tukio.

Dar es Salaam/Nairobi. Ndege kutoka Shirika la Ndege Kenya, imelazimika kutua kwa dharura uwanja wa Stansted wa London badala ya ule wa Heathrow kwa kile kilichodaiwa uwepo wa tishio la kiusalama.

Mtandao wa Daily Nation umeripoti kuwa Polisi nchini Uingereza imethibitisha kuwa, ndge hiyo iliyokuwa ikitokea Nairobi, Kenya kwenda nchini humo, jana Alhamisi Oktoba 12, 2023 saa sita mchana; ilielekezwa kutua katika uwanja wa Stansted.

Ndege hiyo KQ100, ilielekezwa kutua katika uwanja huo ambao ni mahsusi kwa utuaji salama kutokana na kile kilichodaiwa ni tishio la kiusalama, ambapo vyombo vya habari nchini humo, vimeripoti kuwa vikosi vya uteguaji mabomu vimeonekana kukimbilia eneo la tukio.

"Kwa sasa tunaelekea katika tukio Uwanja wa Ndege wa Stansted. Ndege kutoka Nairobi kwenda Heathrow imeelekezwa kutua Stansted mchana wa leo (Alhamisi 12 Oktoba). Uwanja wa ndege bado upo wazi," taarifa ya Polisi wa mji wa Essex katika mtandao wa X, imeeleza.

Katika taarifa hiyo, imedaiwa kuwa shirika  la ndege la Kenya, pia limethibitisha kuwa ndege yake KQ100 kutoka Nairobi hadi London Heathrow, "imepokea tahadhari ya tishio la kiusalama."

"Uongozi wa KQ kwa kushirikiana na mamlaka za usalama katika Serikali ya Kenya na Uingereza,
zimefanya tathmini ya kina ya tishio hilo la kiusalama.

“Wafanyakazi wetu ndani ya ndege walijulishwa juu ya taarifa hizo, huku tahadhari zote za kiusalama zikichukuliwa ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi pamoja na abiria wote ndani ya ndege, wanakuwa salama,” imeleeza sehemu ya taarifa ya shirika hilo la ndege.

Kwa mujibu wa mwandishi wa The Gazette, Daniel Rees, kulikuwa na polisi wengi na kwamba mashuhuda walimueleza kuwa wamewaona wataalam kutoka vitengo vya uteguzi wa mabomu, wakielekea katika uwanja huo wa ndege wa Stansted.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, tukio hilo limetokea siku moja baada kutangaza kuwa baadaye mwezi huu, Mfalme Charles III na mkewe Malkia Camilla watakuwa na ziara ya kiserikali ya siku nne nchini humo.

Rais Samuel Ruto ameialika familia hiyo ya Kifalme nchini humo, wakati taifa hilo likijiandaa kusherekea miaka 60 ya uhuru wake toka kwa waingereza baadaye mwezi Desemba.