Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Somo la ujasiriamali katika desturi za China

Muktasari:

  • Kwa kijana wa Kitanzania, swali la msingi si namna ya kuiga mfumo wa China, bali ni namna ya kuchuja falsafa zao na kuzipandikiza katika ardhi yetu ili kuwa chachu ya kuongeza juhudi zaidi katika kujituma na kuleta matokeo chanya.



Kwa miongo kadhaa, China imepaa kiuchumi na kuwa darasa la dunia kuhusu namna jamii inavyoweza kujinasua kutoka kwenye lindi la umaskini kupitia mageuzi ya kifikra. Hata hivyo, siri ya mafanikio haya haipo tu kwenye korido za serikali au majengo marefu ya Beijing; msingi wake mkuu umelala katika mtazamo wa mwananchi mmoja mmoja kuhusu ujasiriamali, hususan katika ngazi ya biashara ndogo na za kati (MSMEs).

Kwa kijana wa Kitanzania, swali la msingi si namna ya kuiga mfumo wa China, bali ni namna ya kuchuja falsafa zao na kuzipandikiza katika ardhi yetu ili kuwa chachu ya kuongeza juhudi zaidi katika kujituma na kuleta matokeo chanya.

Kwa Wachina biashara inaanza kwa dhamira na msingi mkuu upo kwenye saikolojia ya uanzishaji. Kwa mfano, taarifa za tafiti maarufu zinazofuatilia masuala ya ujasiriamali katika nchi mbalimbali duniani (Global Entrepreneurship Monitor (GEM 2024/25), inaonesha kuwa asilimia kubwa ya wajasiriamali wengi wa Kichina wanaingia kwenye biashara kwa kuona "fursa"

Jambo hili linaweza kuwa kinyume na mazingira yetu, mfano tunayo desturi kuuona ujasiriamali kama "shughuli ya kusitiri aibu" baada ya kukosa kazi ya ofisini. Anayeanza biashara kama karba huwekeza akili, ubunifu, na uvumilivu wa hali ya juu. Lakini anayeanza kama hakuna budi mara nyingi huikatia tamaa biashara mara tu changamoto ya kwanza inapojitokeza, au asiwe mbunifu vya kutosha, au biashara kudumaa kwa mrefu bila kukuwa, na mengine.

Katika mazingira yetu, ikitokea biashara ikifa, mjasiriamali huonekana kama "mshindwa" na hubeba kovu hilo kijamii na kifedha na wakati mwingine hubezwa. Hata hivyo, ripoti za Benki ya Dunia zinaashiria kuwa nchini China, kufunga biashara na kuanza nyingine ni sehemu ya mchakato wa kawaida wa kujifunza.

Mtazamo wa Kichina ni kwamba ikitokea umefunga biashara kwa kushindwa. Jamii inachukulia umeona fursa kwenye biashara nyengine, kwao, itashangaza kama hutaanza kufanya biashara nyingine. Jambo hili kwao inajenga mtizamo mzuri kwamba kushindwa si aibu, mtaji uliopotea ni kama ‘ada ya mafunzo” katika safari ya kuanza biashara nyengine. Ni kama somo ambalo umelilipia kwa gharama ya muda na fedha ili kesho uwe imara zaidi.

Pia jamii ya kachina imejenga na kwa kuamini falfasa ya Guanxi, ambapo katika Nyanja zote za kimaisha huamini maisha ni mtu, familia, watu, kuaminiana, na taarifa nk. Ukichukulia kwa upande wa kibiashara, unaweza kusema ni kama wanaamini kuwa biashara haifanywi na makampuni, bali hufanywa na watu wenye kuaminiana.

Wachina hutumia mitandao ya familia na marafiki kama chanzo cha mtaji, maarifa, taarifa, na masoko. Kwa mfano si lazima yeye awepo Afrika, ila anaweza kuunganishwa kampuni nyengine ije Afrika kwa taarifa na kubadilishana uzoefu. Au kifamilia, wanaweza kuanzisha na kuendesha biashara kwa pamoja, kuunganisha mtaji, kukopeshana nk. Jarida mashuhuri inayofuatilia masuala ya ujasiriamali barani Asia (Asia SME Finance Monitor) inataja kuwa biashara nyingi ndogo za Wachina huanza na mtaji mdogo wa kifedha lakini mtaji mkubwa wa kijamii.

Nchini china kuna dhana kuwa lazima uwe na wazo bora au teknolojia ya hali ya juu ili ufanikiwe, au mashine fulani kubwa uanze kufanya biashara yako. Ingawa wakati mwingine ni kweli, lakini uzoefu katika historia ya maendeleo ya Uchina inaonesha kuwa karakana ambazo zilianza kwa udogo sana ndio ziligeuka kuwa viwanda vikubwa.

Katika mazingira ya biashara ndogo, si lazimakwa kuanza kwa kutengeneza kitu kipya kabisa, bali namna ya kufanya bidhaa iliyopo iwe nafuu zaidi, imara zaidi, au rahisi kutumia. Jambo kubwa la kujifunza kwamba tusisubiri kutengeneza ndege, unaweza kuanza kwa kuboresha ufungashaji wa bidhaa yako ivutie zaidi, kuongeza ubora, kuongeza bidhaa nyengine, na mengine.

Kadhalika mjasiriamali wa Kichina hauzii mteja bidhaa, anauza "suluhisho". Tafiti kwa mfano ripoti ya za watumiaji mtandao (McKinsey & Company 2025 Digital Insights), inaonesha wajasiriamali nchini china wanatumia mitandao ya kijamii kama chombo cha kupata maoni ya wateja na kubadilika haraka (Agility). Unaweza kusema wakiona wateja wanahitaji rangi nyekundu leo, kesho asubuhi bidhaa nyekundu ipo sokoni.

Katika karne hii, mjasiriamali anayechukua siku nzima kujibu ujumbe wa mteja kwenye WhatsApp au Instagram, anajichelewesha. Au pia simu janja na mitandao ya kijamii haipaswi tu kutumika kuweka “post”, ni rada ya kunasa taarifa mpya wateja wanafikiria nini kwa sasa. Ukaribu na mteja ndiyo silaha pekee ya biashara ndogo dhidi ya makampuni makubwa.