Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvutano Holili, wafanyabiashara wafunga barabara

Magari yakiwa yamesimama katika barabara ya Holili-Moshi katika eneo la Holili, wakati wafanyabiashara wa nafaka walipofunga barabara kushinikiza kuondolewa kwa ushuru wa mazao wa Sh300,000. Picha na Omben Daniel

Muktasari:

  • Wafanyabiashara wa nafaka katika mpaka wa Holili Wilaya Rombo, mkoani Kilimanjaro, wamefunga barabara kuu ya Holili-Moshi kwa zaidi ya saa mbili wakishinikiza Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, kuondoa ushuru wa Sh300,000 kwa kila gari lenye mahindi, linaloingia katika Soko la nafaka Holili.

Rombo. Wafanyabiashara wa nafaka katika eneo la mpaka wa Holili, Wilaya Rombo mkoani Kilimanjaro, wamefunga barabara kuu ya Holili – Moshi kwa zaidi ya saa mbili wakishinikiza Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kuondoa ushuru wa Sh300,000 kwa kila gari lenye mahindi linaloingia katika soko la nafaka Holili.

Wafanyabiashara hao waliopanga magari yenye shehena za mahindi, katikati ya barabara katika eneo la Holili na kuzuia magari yanayotoka nchi jirani ya Kenya na yale yanayotokea upande wa Himo, wamesema wamechukua uamuzi huo baada ya kuwepo kwa mabadiliko ya gharama za ushuru, kutoka Sh50,000 hadi Sh300,000, hali inayowaumiza.

Hatua hiyo ilimlazimu Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mwangwala kufika eneo la tukio kuzungumza na wafanyabiashara hao ambapo wamekubaliana kuzuia ushuru huo wa Sh300,000 na kuendelea na ule wa Sh50,000 kwa siku saba ili kupisha mazungumzo kuhusiana na malalamiko hayo.

Wakizungumza leo kwa nyakati tofauti katika soko la Holili, wafanyabiashara hao wamesema kabla ya kufikia Julai 2024, walikuwa wakitozwa Sh50,000 kama ushuru wa mazao wakati wanapotoka sokoni Holili kwenda nchi jirani ya Kenya lakini kwa sasa wameshtushwa na ushuru huo kuongezeka hadi kufikia Sh300,000.

Wamesema mbali ya Sh300,000, pia, wanatozwa Sh10,000 kwa kila gari inayopita bila kujali kama ina mzigo au haina mzigo wakiambiwa ni tozo ya maegesho ya magari huku wakikalamika kutozwa wakiwa wanapita bila kuegesha gari.

Ester Asenga amesema ushuru wa Sh50,000 kwa kila gari waliulipa bila shida lakini kuanzia Jumatano ya Julai 10, 2024 wameanza kutozwa Sh300,000 kiasi ambacho wamekipinga wakidai kuwa kinawaumiza.

“Mimi nina ghala nyumbani kwangu, hivyo nilikuwa nikipita na mahindi yangu sisumbuliwi lakini wakati napakia mzigo nyumbani kwa ajili ya kusafirisha, mtu wa ushuru alikuwa anakuja ananikatia ushuru wa Sh50,000, anaondoka naendelea na safari ilikuwa hakuna shida na mahindi yanayokuja sokoni walileta na saa ya kuondoka wanalipia ushuru huo wa Sh50,000 getini wanaondoka,” amesema Asenga na kuongeza:

“Sasa kikaja kibanda kikawekwa pale barabarani ambacho kimeandikwa madini kikawa kinatoza ushuru wa tofali na pozolana sasa muda si mrefu ghafla tukaona gari zinasimamishwa, kila gari inayopita haijalishi ina mzigo au haina ikawa inatozwa Sh10,000 lakini bango limeandikwa madini, tukaendea nalo, lakini juzi likaja tena hili la Sh300,000, hili linatuumiza wafanyabiashara.

Naye Zuberi Hamis amesema: “Tuko hapa kwa tukio ambalo limetushangaza, tumeambiwa gari ikitoka huko ilikotoka ikifika hapa Holili ilipe Sh300,000, tunauliza fedha hizo ni za nini kwa sababu gari iko barabarani, haijajulikana hata inapokwenda kama ni Mombasa, sokoni, au wapi, wao wanataka Sh300,000 sasa hiyo fedha hakuna mtu ambaye anaweza kulipa.”

Amehoji: “Sasa tunasema fedha hizi hatuwezi kulipa, kwani hata hilo soko hapo lipo tu, halina vyoo, maji wala ustaarabu wowote wa soko lakini tunatozwa ushuru, leo tunakuja tunaambiwa kila mtu alipe Sh300,000, sasa kama hapa tutatozwa Sh300,000, himo hivyo hivyo na Moshi tena Sh300,000, tutakaa barabarani kweli?”

Solomon Kippa amesema: “Sheria ya leseni inaturuhusu kulipa mapato ya Halmashauri pale tunapopakia mzigo na usipate usumbufu wowote mpaka unapofika mwisho wa safari, lakini hapa Rombo imekuwa ni tofauti leo ni siku ya pili magari yamelala hapa na polisi wanayalinda, sasa tunachoomba hili suala litafutiwe ufumbuzi leo kwani linatuumiza".

Akijibu malalamiko hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rombo, Godwin Chacha ambaye aliongozana na Mkuu wa Wilaya kufika eneo hilo, amesema wamepokea kero hizo na kwamba watakaa na wafanyabiashara hao ili kutafuta suluhisho. 

“Mkuu wa Wilaya, sisi tumepokea hizi kero zao lakini kwa mujibu wa sheria za masuala ya mazao na sisi tunakaguliwa, walifanya utafiti wenzetu wa CAG waliangalia mazao ya aina mbili, waliangalia viazi na mahindi, tuna hoja pia kwa sababu nchi inafuata sheria na taratibu.”

Ameongeza kuwa: “Lamda kitu ambacho tunaweza tukasema ukituruhusu sisi bado tuna nafasi ya kukaa nao na tukahakikisha tunafikia mwisho, kwani tumekaa nao vikao vingi sana kuhusiana na soko hili na wameshiriki katika kulikuza.”

Amesema watafanya vikao mfululizo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa na yale watakayokubaliana watapeleka taarifa, kwa kuwa hawataki mfanyabiashara aumie, kwa kuwa halmashauri inawategemea wao.

Akizungumza mkuu huyo wa wilaya amewataka wafanyabiashara kuwa na subira na kutoa siku saba kwa watendaji wa halmashauri kukaa na wafanyabiashara kuzungumza ili kupata suluhusho la malalaniko hayo.

“Poleni kwa yote ambayo yamewasibu kuanzia jana na wengine kuanzia juzi lakini pili niwashukuruni sana kwani tumezungumza na kupata picha iliyo sahihi, niombe halmashauri jengeni uhusiano mzuri na wafanyabiashara kwa sababu ndiyo wadau wetu,” amesema.

“Niwaombe kama mlivyotuvumilia hapa, muendelee kutuvumilia, nikupe kazi mkurugenzi na timu yako muone picha ilivyo, muangalie utekelezaji mzuri unaweza ukawaje, maana mnaweza kukuta mko sawa lakini watu hawana taarifa, zoezi limetekelezwa wakati mwananchi hana taatifa, wamekutana nalo likawashtua.