Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maonyesho sabasaba hadi saa mbili usiku

Muktasari:

  • Mda umeongezwa ili kutoa nafasi zaidi kwa waonyeshaji na watembeleaji ili waweze kutumia muda wa ziada.

Dar es Salaam. Ikiwa zimebaki siku mbili kabla ya maonyesho ya 49 ya biashara ya Dar es Salaam kuanza, muda wa uonyeshaji bidhaa kwa wazawa umeongezwa kutoka saa 12 jioni hadi saa 2 usiku. 

Hata hivyo hakuna mabadiliko ya muda kwa waonyeshaji wa kigeni huku muongozo wa ongezeko hilo la muda ukitarajiwa kutolewa vizuri maonyesho yatakapoanza.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) Latifa Khamis mbele ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila baada ya kumaliza ukaguzi wa maandalizi ya mwisho.

Latifa amesema katika maonyesho ya mwaka huu mambo mengi yamefanyika kisasa ikiwemo uchaguaji na ulipiaji wa mabanda ambapo watu waliweza kufanya kidigitaki bila kulazimika kwenda ofisini.

“Suala la tiketi mwaka jana tulitumia kampuni moja ya simu watu kununua tiketi lakini mwaka huu mitandao yote itatumika kununua tiketi,” amesema Latifa.

Akielezea kilichoongezeka mwaka huu, Latifa amesema kutakuwa na vijiji mbalimbali ikiwemo kile cha ya Wizara ya Habari Sanaa na Michezo ambapo ndani yake kutakuwa na burudani mbalimbali zinazohusisha wasanii.

Pia kutakuwa na vikundi mbalimbali vya burudani vitakavyokuwa vikitumbuiza kupitia ratiba maalumu zitakazotolewa.


Pia kutakuwa na Kijiji cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambapo timu mbalimbali za mpira zitakuwepo ikiwemo Yanga, Simba, Namungo, Azam ambapo programu mbalimbali zitawekwa ili watu waweze kufurahia uwepo wake.

Timu hizo zitakuwa na vikombe vyote walivyochukua ili kutoa fursa kwa watembeleaji kupiga navyo picha.

“Kwa upande vijiji kutakuwa na saa za ziada hadi saa 4 hadi 5 usiku na wale wanaotoka nje wataonyesha hadi saa 12, waonyeshaji wa ndani wataongezewa muda hadi saa 2 usiku na utaratubu mzuri tutawapa kuanzia siku ya kwanza muweze kuelewa,” amesema.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema maonyesho ya biashsra ya kimataifa ya Dar es Salaam 

Amesema Dar es Salaam ni mkoa kama mingine lakini ukiwa umejaaliwa kuwa na bandari iliyofanyiwa uwekezaji ambayo inaweza kuhudumia nchi mbalimbali ambazo hazina bahari.

Amesema nchi ambazo hazina bandari zinaitazama Tanzania kama nchi inayozisaidia kujiendesha.

Maonyesho ya biashara ya kimataifa yanapofanyika Dar es Salaam si kwa bahati mbaya bali ni sehemu ambayo watu wengi wanaweza kufika na kuhudumiwa na kufanya mambo makubwa.

“Tunapozungumzia kupima pato la taifa na kiwango cha uamasikini biashara ni kitu muhimu kinachoweza kutupa matokeo chanya kuonyesha ukuaji wetu kiuchumi na kupunguza umasikini hivyo maonyesho haya yanapofanyika husaidia kuchochea ukuaji wa pato la Taifa,” amesema.

Amesema hilo linaenda sambamba na kulinda usalama wa Taifa kwani sasa haulindiwi kwa bunduki pekee ila mambo mengi ikiwemo kuangalia usalama wa chakula, mazingira mazuri salama.

“Taifa likiwa halina chakula ni rahisi kukosa utulivu wa kiasia kwa sababu watu wana njaa, ukiharibu mazingira leo taifa linakuwa katika nafasi ya kuingia katika machafuko ya kisiasa,

“Tutaanza kushuhudia matatizo ya kisiasa kama yanayoendelea katika nchi nyingine kwa sababu tumeharibu mazingira ambayo madhara yake ni kukosekana kwa mvua, chakula, maradhi kuwa mengi na taifa maskini,” amesema.

Aliwataka wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kutobaki kusifu maonyesho hayo wakiwa wamelala kitandani na badala yake wawe sehemu ya maonyesho.

Amesema maonyesho hayo ni kielelezo cha diplomasia na uhusiano wa kimataifa uliopo kati ya Tanzania na mataifa yatakayoshiriki katika maonyesho hayo.

Uhusiamo huo utajikita katika sera ya mambo ya nje iliyozinduliwa hivi karibuni inayoonyesha Tanzania itafanya nini katika mahusiano hayo.

“Tukisema ni kielelezo cha diplomasia na uhusiano wa kimataifa ya nchi zetu maana yake maonyesho haya yanapaswa kuwa ya kimataifa.


Mkuu wa wilaya ye Temeke, Sixtus Mapunda amesema maonyesho ya mwaka huu yako vizuri ukilinganisha na mwaka uliopita.

Amesema wamejipanga kupitia sekta mbakimbali ikiwemo usalama kwani washiriki watalindwa kwa nguvu zinazoonekana na zisizoonekana.

“Ni zaidi ya akili unde zinaweza kukuona hata bila camera hata ukiwa Sumbawanga, utaratibu wa usafirishaji wa mizigo ya washiriki  mikoani itatumia utaratibu maalumu, wale wanaobeba mizigo na mafuso na lumbesa sasa hayatakuwapo kwani kuna utaratibu maalumu umeandaliwa,” amesema.