Hifadhi sasa yajenga barabara kuunganisha Selous, Mikumi

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Tanzania, Teddy Mapunda akiwagawia soda wanafunzi wa shule ya sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya Wama-Nakayama iliyopo Kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakati wa sherehe za Sikukuu ya Eid. Picha na Anna Nkinda
Muktasari:
- Alisema kuwa lengo la kufungua barabara hiyo ni kuwaunganisha watalii waweze kufika katika Hifadhi ya Mikumi kupitia upande wa Kusini mwa hifadhi hiyo maeneo ambayo hayajawahi kutumika kwa utalii pamoja na kuwa na vivutio vingi adimu.
Morogoro. Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Datomax Selanyika amesema wameanza ujenzi wa barabara itakayounganisha Pori la Akiba la Selous na hifadhi hiyo lengo likiwa ni kuwarahisishia watalii wanaotaka kufika katika hifadhi hizo kutumia muda mfupi zaidi.
Alisema barabara hiyo itakuwa na umbali wa kilomita 143 ukilinganisha na mzunguko uliopo sasa wa kutoka Selous kupitia Kisaki, Mvuha, Matombo hadi Morogoro mjini ndipo ufike Mikumi umbali wa kilomita zisizopungua 248.
Selanyika alisema hayo jana wakati akizungumza mjini Morogoro ambapo alisema kuwa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.
Alisema kuwa lengo la kufungua barabara hiyo ni kuwaunganisha watalii waweze kufika katika Hifadhi ya Mikumi kupitia upande wa Kusini mwa hifadhi hiyo maeneo ambayo hayajawahi kutumika kwa utalii pamoja na kuwa na vivutio vingi adimu.
“Asilimia 30 ya Hifadhi ya Mikumi ndiyo inatumika kwa utalii kwa sasa, asilimia 70 ilikuwa bado haijafunguka bado ni mapori mazito, kufunguliwa kwa barabara hiyo kutasaidia watalii kuona vivutio vingi,” alisema.
Mhifadhi huyo alisema kujengwa kwa barabara hiyo kutahamasisha watalii wengi wa ndani na nje ya nchi kufurahia kutembelea maeneo hayo na kwamba wamejipanga kutoa huduma zitakazohitajika wakati wote.