Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BoT yapigia chapuo matumizi kazi za mikopo

Muktasari:

  • Uzinduzi wa Absa Infinite Card ni matokeo ya msingi wa mafanikio ya benki ya Absa tangu mwaka 2015, ilipoanzisha kadi ya kwanza ya mikopo, ikishirikiana na mtandao wa Visa.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema kuna fursa ya kuendeleza matumizi ya bidhaa za kadi za mikopo, hivyo imehimiza benki nchini kuwekeza zaidi katika ubunifu na elimu kwa wateja.

Aidha, BoT imeipongeza Benki ya Absa Tanzania kwa kuzindua (Absa Infinite Card), kadi ya kifahari inayolenga kuwahudumia wateja wa hadhi ya juu kwa huduma za kifedha zilizoboreshwa na zenye uzoefu.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, ambapo Absa imeadhimisha miaka 10 ya utoaji wa kadi za mikopo (credit card), Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Kitaifa kutoka BoT, Lucy Charles-Shaidi ameipongeza Absa kwa kuendeleza ubunifu huo wa kidijitali.

“Bidhaa za kadi ya mikopo bado ni ngeni kwa Watanzania wengi. Tunazihimiza benki kuwekeza zaidi katika ubunifu na elimu kwa wateja ili kuchochea matumizi sahihi,” amesema Lucy aliyemwakilisha Gavana wa BoT.

Amesema Benki Kuu itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuendeleza ujumuishaji wa kifedha na matumizi ya teknolojia za kisasa za malipo.

Uzinduzi wa Absa Infinite Card ni matokeo ya msingi wa mafanikio ya benki ya Absa tangu mwaka 2015, ilipoanzisha kadi ya kwanza ya mikopo, ikishirikiana na mtandao wa Visa.

Absa Infinite Card inapatikana kwa njia ya kadi ya kawaida ya benki na kadi ya mkopo inatolewa kwa pesa ya Tanzania na Dola za Marekani.

Kadi hii imebuniwa kukidhi mahitaji ya wateja wanaotafuta ubora, usalama na upatikanaji wa huduma duniani kote.

Miongoni mwa faida zake ni bima ya safari za kimataifa, kupata huduma za chakula, vinywaji na mapumziko katika viwanja vya ndege zaidi ya 1,200, bei ya punguzo katika manunuzi, bima ya kufuta tiketi za safari na udhamini wa bidhaa za muda mrefu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Bank Tanzania, Obedi Laiser amesema kadi hiyo inaakisi mahitaji ya Watanzania wanaotamani huduma bora za kifahari za benki.

 “Tunafanya uwekezaji mkubwa katika elimu kwa wateja ili kuhakikisha Watanzania wanaelewa thamani ya usalama, urahisi na faida zinazotolewa na kadi za mikopo,” amesema.

Mkurugenzi wa Huduma za Wateja wa Rejareja wa Absa, Ndabu Swere, amesema nguvu ya benki hiyo haiko tu kwenye bidhaa, bali pia kwenye watu wanaotoa huduma hizo.

“Kwa kadi ya Infinite, wateja wetu hawapati tu kadi, bali wanapata uzoefu wa huduma binafsi, unaoendeshwa na timu iliyojitolea kuwahudumia kwa viwango vya kimataifa,”

Kwa hatua hii, Benki ya Absa Tanzania inaendelea kusisitiza dhamira yake ya “Kuiwezesha Afrika ya kesho, stori moja baada ya nyingine,” ikilenga kuimarisha ushirikishwaji wa kifedha na kuchochea maendeleo ya sekta ya kibenki kwa ubunifu na huduma bora.