Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zuchu kakosa tano, kapata tano 2023

Muktasari:

  • Baada ya kuvikosa vipengele vitano vya Soundcity MVP, Mei mwaka huu Zuchu alishinda vipengele vitano vya tuzo za muziki Tanzania (TMA) 2022 na ndiye msanii pekee aliyefanya vizuri zaidi.

Ikiwa ni miaka mitatu tangu staa wa Bongofleva, Zuchu kutoka kimuziki chini ya WCB Wasafi, mwaka huu ndipo ameshinda tuzo nyingi zaidi kwa mpingo na vilevile kukosa nyingi.

Utakumbuka Zuchu ni msanii wa pili wa kike kusainiwa WCB Wasafi baada ya Queen Darleen aliyesainiwa mwaka 2016 pamoja na Rich Mavoko, ila kwa sasa ni msanii wa pili wa lebo hiyo aliyefanikiwa zaidi kimuziki baada ya Diamon Platnumz.

Zuchu alitajwa kuwania vipengele vitano katika tuzo za Soundcity MVP Awards zilizotolewa Februari mwaka huu huko Lagos, Nigeria, matumaini ya ushindi yalikuwa ni makubwa kwa kutazama idadi ya vipengele alivyopendekezwa ila haikuwa hivyo.

Alitajwa kuwania Soundcity MVP kama Msanii Bora Afrika, Msanii Bora wa Kike, Msanii Bora wa Digitali, huku wimbo 'Mtasubiri' akishirikishwa na Diamond ukiwania kama Wimbo Bora wa Pop na Video Bora.

Licha ya kuhudhuria na kutumbuiza katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo, Zuchu alirudi nyumbani mikono mitupu sawa na Phina ambaye naye alitumbuiza huku akiwania kipengele kimoja cha Msanii Bora Chipukizi.

Waliomzidi kete Zuchu ni Burna Boy (Msanii Bora Afrika), Tems (Msanii Bora wa Kike), Rema (Msanii Bora Digitali), huku wimbo 'Peru Remix' wa Fireboy DML ft. Ed Sheeran ukishinda kama Wimbo Bora wa Pop, na Video Bora ikienda kwa Fireboy x Asake (Bandana)

Utakumbuka kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Nahreel na Aika ndio wasanii wa mwisho kutokea Tanzania kushinda Soundcity MVP Awards ambapo mwaka 2019 walishinda kama Kundi Bora la Mwaka.

Baada ya kuvikosa vipengele vitano vya Soundcity MVP, Mei mwaka huu Zuchu alishinda vipengele vitano vya tuzo za muziki Tanzania (TMA) 2022 na ndiye msanii pekee aliyefanya vizuri zaidi.

Zuchu alishinda kama Msanii Bora wa Kike wa Mwaka, Video Bora ya Mwaka (Mwambieni), Msanii Bora wa Kike Bongofleva, Wimbo Bora wa Bongofleva (Kwikwi) na Mwanamuziki Bora wa Kike Chaguo la Watu Kidigitali

Ikumbukwe tuzo za TMA zilizoanzishwa mwaka 1999 na Baraza la Sanaa Taifa (Basata), ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa Zuchu kuwania baada ya mwaka 2021 ziliporejea lebo yake kususia tuzo hizo kwa madai ya kutoridhishwa na mchakato wake mzima.