Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zaiid: Wimbo 'Tafuta Bwana' haujalenga wanawake pekee

Muktasari:

  • Zaiid amesema wimbo huo una maana ya watu kumtafuta Bwana Mungu, vijana kujua umri unaenda watafute pesa na wanawake wapunguze udunia watafute mabwana wa kuwaoa.

Dar es Salaam. Msanii wa Hip Hop nchini Zaiid amesema wimbo wake wa 'Tafuta Bwana' unaotamba kwa sasa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, umebeba engo tatu, ingawa jamii imepokea kwa upande wa wanawake.

Zaiid amesema wimbo huo una maana ya watu kumtafuta Bwana Mungu, vijana kujua umri unaenda watafute pesa na wanawake wapunguze udunia watafute mabwana wa kuwaoa.

Alifafanua kipande cha wanawake kuwa tofauti na miaka ya nyuma ambayo walikuwa na staha, utulivu na sikio la kusikiliza, tofauti na sasa ambapo wanaongea sana katika mitandao ya kijamii na kushindwa kujistiri, jambo linalowarudisha nyuma wanaume wengi kufanya maamuzi ya kuoa.

"Mfano mtaa kwetu huku changanyikeni huu ni mwaka wa pili, sijaona  gari la harusi likipita, unaweza ukapata picha ni namna gani maadili ya zamani yanavyoporomoka, vijana hawaoni umuhimu wa ndoa tena," alisema na kuongeza.

"Wimbo huo niliurekodi miaka minne iliyopita, ulitokana na mshikaji wangu producer RingoBeats akawa amerekodi kama kichekesho akakituma kwangu. Nikamwambia ni kizuri unaonaje tukifanyie wimbo, akasema kila kitu unataka wimbo vingine vikupite.

"Sikukata tamaa baada ya siku tatu nikaenda studio nikamkuta hana kazi nyingi, hivyo akakubali kurekodi kishingo upande, namna alivyoingia, Belle 9 ambaye ni mshikaji wangu sana, alinipigia simu kwamba tufanye kazi ya pamoja, akaja tukaenda studio.

"Producer akawa amechelewa kufika, wakati tunamsubiri nikaanza kupiga nyimbo zangu nilizorekodi ilipofika wa Tafuta Bwana, Belle9 akasema huohuo nikafuta vesi yangu ya pili akaingiza sauti yake, naona jamii imeupokea vizuri, ila nasisitiza una engo tatu haujalenga wanawake pekee.