Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utofauti wa Bongo Movie ya sasa na ile ya Kaole

Muktasari:

  • Nina na Kisa pamoja na Nora. Wale walikuwa wenye dhamira na vipaji vya kweli. Waliingia kwenye sanaa kwa wito na vipaji vya kweli. Hakuna kati yao aliyewaza kuendesha gari wala kupanga jumba la mamilioni

Dar es Salaam. Bongo movie ya Kaole wengi wao waliingia kwenye sanaa kwa kuipenda sana. Hawakuwa na ndoto ya utajiri wa umaarufu. Ndiyo. Bishanga hakuwaza ustaa na utajiri. Ustaa ulikuja kutokana na ubora wake wa kazi. Ndo maana ubunifu ulikuwa mkubwa. 

Nina na Kisa pamoja na Nora. Wale walikuwa wenye dhamira na vipaji vya kweli. Waliingia kwenye sanaa kwa wito na vipaji vya kweli. Hakuna kati yao aliyewaza kuendesha gari wala kupanga jumba la mamilioni.

Kina Ommy, Kalunde, Kemmy, Waridi na Mashaka. Ni kundi flani la watu waliozaliwa kuja kuigiza duniani. Ndo maana walifanya sanaa  kwa kiwango cha juu bila mamilioni kwenye benki akaunti zao. Nammisi Mzee Small na Pwagu.

Sanaa ya sasa siyo mbaya, lakini vipi kuhusu vipaji na weledi wa fani? Vipi kuhusu mafunzo katika jamii kama kusudio la sanaa? Enzi  za Kibakuli na Nyamayao sio zamani sana wakati tunaona kazi zao. Namisi nyakati zao. 

Tumepoteza maigizo yenye uhalisia. Vipaji vya uhakika na hadithi tamu za kibunifu. Zenye kutoa funzo kwa jamii. Naimisi Kaole iliyowatoa Dk Cheni na Swebe. Sinta na Lulu, Johari, Ben na Ray Kigosi. Namisi nyakati zao.

Naimisi Splendid ya Billy na Migomba, Mau, Dude na Chekibudi. Waliifanya sanaa bila uwekezaji  mkubwa ila waliacha alama za kukumbukwa. Yes! Natasha na mwanaye Monalisa pindi akiwa binti mdogo. Namisi wakati ule.

Sasa hivi tunakodi jumba la kifahari. Tunashindwa kupata wasaniii wenye vipaji halisi. Wapi Kipemba? Christant Muhenga ni lini tunapata ile raha ya sanaa ya uigizaji kama zamani zile? Napamisi hata Lango la Jiji.

Nyakati zinaenda hazirudi. Walio hai tumshukuru Mungu. Waliotangulia, Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa pumziko jema la milele. Nakumbuka Dar es Salaam ya Mambo hayo na Kaole Sanaa Group.