Rick Ross kujiandalia makazi ya siku ya mwisho chini ya ardhi

Muktasari:
- Kupitia video inayosambaa mitandaoni ikimuonyesha Rick akieleza kuwa atajenga chumba hicho kwa lengo la kujiandaa na maisha yake ya siku ya mwisho.
Dar es Salaam. ‘Rapa’ kutoka nchini Marekani Rick Ross ameweka wazi kuwa ana mpango wa kujenga nyumba chini ya ardhi ambayo itakuwa na chumba cha kulala, gereji na mashine inayotengeneza maji kutoka angani.
Kupitia video inayosambaa mitandaoni ikimuonyesha Rick akieleza kuwa atajenga chumba hicho kwa lengo la kujiandaa na maisha yake ya siku ya mwisho.
Mbali na kutaka kujenga mjengo huo, Rick pia anamiliki ndege binafsi (private jet), eneo la hekari 2.3 kwa ajili ya mapumziko lililopo Florida, na Jumba la kifahari la ‘Star Island Waterfront'.
Ikumbukwe pia baadhi ya matajiri dunia kama vile Elon Musk na Mark Zuckerberg tayari wamejenga nyumba za chini ya ardhi, zijulikanazo kama ‘Bunkers’ ambazo kwa kawaida hugharimu zaidi ya Dola 38,000, (Sh95.5 milioni) kulingana na ukubwa wa eneo.
Lakini endapo ikiwa kubwa zaidi inaweza kufikia Dola 60,000 (Sh150.9 milioni).