Album ya Rick Ross kawashilikisha wakali kibao

Muktasari:
- Albamu ya Rick Ross itatoka Agosti 9, 2019 ikiwa na nyimbo 15 alizowashirikisha mastaa wakali akiwemo Drake, Jeezy, Swiss Beatz, Meek Mill, Denzel Curry, Ball Greezy na Dej Loaf
Marekani. Rapa Rick Ross ametaja majina ya wasanii watakaosikika kwenye albamu yake ya 10 iitwayo ‘Port of Miami 2’ itakayotoka Agosti 9, 2019.
Albamu hiyo ni mwendelezo wa albamu ya ‘Port Of Miami’ iliyotoka 2006 ikiwa na ngoma 15 ikiwamo aliyofanya na marehemu Nipsey Hussle ‘Rich Nigga Lifestyle’ pamoja na Teyana Taylor.
Wasanii wengine watakaotikisa kwenye albamu hiyo ni Drake, Jeezy, Swiss Beatz, Meek Mill, Denzel Curry, Ball Greezy na Dej Loaf.
Kwa mujibu wa tovuti ya RollingStone singo ambazo zinajulikana ni pamoja na “Gold Roses” aliomshirikisha Drake, “Big Tyme” aliomshirikisha Swizz Beatz na “Act a Fool” aliofanya na Wale.