Mr Nice ndani ya Bongo Fleva Honors 2024

Muktasari:
Mkurugenzi wa Tamasha la Bongo Fleva Honors, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amesema msimu wa pili wa tamasha hilo utaanza Januari 26, 2024
Mwanamuziki wa Hip-Hop ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tamasha la Bongo Fleva Honors, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, jana Januari 15, 2024 ametangaza ujio wa msimu wa pili wa tamasha, huku ndani akiwamo mwanamuziki Lucas Mkenda (Mr Nice).

Sugu amesema msimu wa pili wa tamasha hilo utaanza Januari 26, 2024 na Nice kuwa ndiye atafungua kwa mwaka huu. Msimu wa kwanza ulianza Januari 2023 na kumalizika Novemba, 2023.