Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mr Nice:  Muziki? Mi nachora balaa

Muktasari:

  • Ni alama isiyofutika kwenye muziki Bongo Fleva kutokana na mchango aliouweka, ikiwemo kufanya ngoma kali kama Kikulacho, Fagilia na nyingine nyingi.

Dar es Salaam, Wegi wa kizazi cha miaka ya 2000 wameishia kusikia tu jina Mr Nice lakini hawajui maisha yake ya muziki na nje ya kazi hiyo.

Ni alama isiyofutika kwenye muziki Bongo Fleva kutokana na mchango aliouweka, ikiwemo kufanya ngoma kali kama Kikulacho, Fagilia na nyingine nyingi.

Majina yake kamili ni Lukas Mkenda na alitamba na staili yake ya TAKEU akimaanisha Tanzania, Kenya, Uganda na kulishika soko la muziki Afrika Mashariki miaka ya 2000.

Kama kawaida Mwanaspoti kupitia safu yake ya 'Dakika 5 Na...' lilimnasa na hakusita kutoa ushirikiano kujibu maswali ya mwandishi na kubwa alilofunguka na wengi hawajui, mbali na kuimba, anajua sana kuchora na kufunguka mambo ya hela na zilipoanzia.

Mwananchi: Ni watu hawakijui kutoka kwako?
 

Mr Nice: Kazi yangu kubwa ni kuchora, nachora michoro ya aina yote. Watu, wanyama, ndege na vingine vingi. Tena mimi najua kuchora kuliko muziki, nawaambia watu nimeanza kushika pesa kitambo kabla sijaingia kwenye muziki.

Mwananchi: Bado unafanya muziki Kenya?
 

Mr Nice: Ndiy. Nimeamua kuhamishia shughuli zangu za muziki Kenya kwa sababu watu wa Tanzania hawataki tena muziki wangu, afadhali Wakenya. Nyimbo wanazopenda kusikiliza Watanzania sasa hivi ni mapenzi, matusi hadi kufungiwa na Basata.

Mwananchi: Vipi Maisha yako ya sasa na ya zamani?
 

Mr Nice: Maisha yangu ya sasa ni mazuri tofauti na nilipofilisika nikiwa Tanzania, yalikuwa mabaya sana, sasa hivi nimerudi Mr Nice wa zamani.

Mwananchi: Kipindi unawika ulikuwa na bifu na wasanii wenzako, ni kweli?
 

Mr Nice: Nilikuwa mkorofi sababu nilikuwa na pesa nyingi sana kipindi hicho, hivyo nilikuwa nadhani naweza kufanya kila kitu, maugomvi, starehe, ubabe na mambo mengine mengi ya ovyo, ila sijawahi kuwa na bifu na wasanii wenzangu kwani mimi nilikuwa naimba muziki wa aina tofauti na wao.

Mwananchi: Nyimbo zako nyingi zilipendwa na watoto, nini siri?
 

Mr Nice: Ukweli mimi nilichokuwa naimba ni Mungu ndiye anajua, sababu sikuwa nimepanga kuimba nyimbo za aina ile na kufikiria kupendwa na watoto, mimi nilikuwa naimba Kwaya Kanisani, kwa hiyo nikaona kuimba Rap, RnB na muziki mwingine siwezi, sasa nikajikuta tu naimba muziki wa aina ile na zile staili za TAKEU zilikuwa zinatokea na nashukuru zilipendwa na mashabiki zangu.

Mwananchi: Kitu gani hukipendi?
 

Mr Nice: Watanzania kujifanya wamesahau nyimbo zangu wakati walikuwa wanaburudika nazo. Yaani kwa hiki kinachoendelea ningebaki kuishi Tanzania ningeweza kufa kwa stresi. Pia sipendi majungu na uzushi.

Mwananchi: Nani walikuwa washindani wako kwenye muziki?
 

Mr Nice: Mimi bwana sikuwa nafanya muziki wa mashindao ila kuna wanamuziki ambao walikuwa wanafanya muziki wa aina yao na tulikuwa tunawika kwa pamoja, alikuwepo Juma Nature, Crazy GK, Inspector Haroun hawa nilipambana nao hadi nikatoboa kwenda nje ya nchi wao walibakia kuwaimbia Watanzania.

Mwananchi: Unawashauri nini wasanii wa sasa?
 

Mr. Nice: Wafanye muziki mzuri waache kufanya kiki kupitia kazi zao, kwani unaweza kutoboa bila kiki. yaani utakuta mtu eti anafanya kiki ya kujiua, mara ajali mara nini yaani huwa nawashangaa sana na kujiuliza uwezo wao ndio umeishia hapo kweli?.