Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpango wa Marioo kumuoa Paula upo hivi...

Muktasari:

  • kwa upande wake Marioo akizungumza katika mahojiano hayo amesema mipango ya kumuoa Paula tayari imefanyika hivyo siku yoyote atatangaza tarehe

Dar es Salaam. Paula Paul ambaye ni mtoto wa mwigizaji Kajala Masanja, na Mzalishaji muziki P Funk Majani, amesema yupo kwenye mpango wa kurudi shule kujiendeleza na masomo huku akikazia kuwa endapo ndoa ikitangulia litakuwa jambo zuri zaidi.

"Nalipokea kwa kawaida jina la Paula sitaki shule, ni fikra zao wenyewe, napotezea. Nina mipango ya kuendelea na shule, nasubiri Amara akue. Nataka kuendelea kusomea fashion kwa sababu ndiyo kitu ambacho napenda, nataka kujiendeleza kwenye hilo," amesema Paula Novemba 25, 2024 wakati akifanyiwa mahojiano na Clouds Media.

Aidha amesema endapo Marioo akitaka kumuoa yupo tayari kuolewa kwanza ndiyo asome.

Hata hivyo, kwa upande wake Marioo akizungumza katika mahojiano hayo amesema mipango ya kumuoa Paula tayari imefanyika hivyo siku yoyote atatangaza tarehe.

"Sisi tupo kama familia suala la ndoa ni dogo sana, ni kuamua na sheria tumeanza kufuata, mambo ya msingi tumeshafanya imebakia suala la kusema tarehe fulani tunataka kuoana, mpango huo upo kwa sababu nampenda, amenizalia mtoto mzuri kwa hiyo kama hitaji lake ni ndoa ni dogo sana barua tulishapeleka," amesema Marioo. 

Paula hakuacha kuzungumzia mitazamo ya watu juu ya malezi anayopata kwa mama yake huku wengi wakidai wawili hao hawaheshimiani.

"Sisi tuna mipaka, hatupo kama watu wanavyotuona, alikuwa hadi ananipiga, mara ya mwisho amenipiga nikiwa na miaka 18. Alikuwa mkali japo sasa hivi siyo kama mwanzo ananielewesha naelewa," amesema.