Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mke asimulia dakika za mwisho za Lundenga

LUNDENGA Pict

Muktasari:

  • Lundenga aliyekuwa mkurugenzi wa Lino Internation Agency,  waandaaji wa Miss Tanzania tangu 1994 hadi 2018 amefariki jana baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Dar es Salaam. Twigi Lundenga ambaye ni mke wa Hashim 'Anko ' Lundenga ameeleza dakika za mwisho za mumewe.

Amesema Lundenga alikata kauli akiwa ICU miezi minane iliyopita.

Lundenga aliyekuwa mkurugenzi wa Lino Internation Agency,  waandaaji wa Miss Tanzania tangu 1994 hadi 2018 amefariki jana baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mwili wake utazikwa Jumanne, nyumbani kwao Kidatu huko Kilombero mkoani Morogoro, kesho Jumatatu utasafirishwa kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Morogoro tayari kwa maziko.

Akielezea dakika  za mwisho  za mumewe, Twigi amesema Lundenga alikata kauli tangu Agosti mwaka jana.

"Hali yake ilikuwa mbaya alikuwa anakula kwa mpira wa tumboni," amesema Twigi kwa huzuni na kuendelea.

"Alitobolewa utumbo mkubwa ili kupitisha chakula kutokana na hali yake kuwa mbaya hadi mauti ilipomkuta jana.

Akielezea ugonjwa uliomtesa mumewe kwa muda mrefu, Twigi amesema alikuwa akisumbuliwa na stroke.

"Ilikuwa inajirudia mara kwa mara, Agosti mwaka jana akiwa ICU ndipo alikata kauli, hadi mauti ilipomkuta," amesema .

Twigi amesema kipindi hicho pia mfumo wa Lundenga wa mzunguko wa damu kwenye moyo ulikuwa hauna nguvu.

"Mume wangu ameteseka, tulipambana kumuuguza, lakini Mwenyezi Mungu amempenda zaidi, kikubwa tunamuombea," amesema Twigi.

Akizungumzia taratibu za maziko ya muasisi huyo wa shindano la Miss Tanzania lililopata umaarufu miaka ya nyuma, Twigi amesema mwili wake utasafirishwa Jumatatu jijini Dar es Salaam.

"Mazishi yatakuwa Jumanne, nyumbani Kilombero, huko Kidatu, Jumatano baada ya mazishi tutakuwa kule na Alhamisi tutarejea Dar es Salaam kuendelea na matanga nyumbani Bunju," amesema.

Lundenga alikuwa muandaaji wa Miss Tanzania tangu mwaka 1994 hadi 2018 alipokabidhi kijiti kwa Basilla Mwanukuzi, ambaye anaendesha shindano hilo hadi sasa.

Moja ya mafanikio akiwa muaandaji wa shindano hilo ni Tanzania kutwaa taji la Miss World Afrika kwenye mashindano ya dunia.