Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Michael Jackson apata wa kufanana naye

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa muongozaji Antoine Fuqua na mtayarishaji Graham King wa filamu hiyo, wameeleza kuwa japo Jaafar ana uwezo mdogo katika uigizaji lakini ndiye mtu pekee ambaye amebeba uhusika wa MJ ipasavyo, hivyo wanafuraha sana kumfufua mwanamuziki huyo katika tasnia ya uingizaji.

Marekani. Kutokana na kuwepo kwa mpango wa kutengenezwa filamu ya mfalme wa Pop Michael Jackson (MJ), huku akisakwa mtu ambaye atafanana naye miondoko kama msanii huyo, hatimaye mtu huyo amepatikana ambaye ni Mpwa wa MJ aitwaye, Jaafar Jackson.

Kwa mujibu wa muongozaji Antoine Fuqua na mtayarishaji Graham King wa filamu hiyo, wameeleza kuwa japo Jaafar ana uwezo mdogo katika uigizaji lakini ndiye mtu pekee ambaye amebeba uhusika wa MJ ipasavyo, hivyo wanafuraha sana kumfufua mwanamuziki huyo katika tasnia ya uingizaji.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Jaafar ame-share picha ambazo zinamuonesha akiwa kwenye mapozi ya MJ, akiambatanisha na ujumbe ukieleza kuwa ni furaha na heshima kubwa kwake kutekeleza uhusika wa mjomba wake Michael.

Filamu hiyo ya ‘Michael’ ilipangwa kuaza kurekodiwa mwaka 2023 lakini kufuatiwa na changamoto, imeanza kurekodiwa mwishoni mwa Januari 2024, huku ikitarajiwa kuachiwa rasmi Aprili 18, 2025.

Jaafar Jackson (25) ni mwanamuziki na dansa ambaye alianza kuimba rasmi akiwa na umri wa miaka 12 na kujulikana rasmi mwaka 2019, baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Got Me Singing’, huku wimbo wake wa mwisho akiwa ameachia jana Februari 14 uitwao, ‘Rebirth of Michael’.

Ikumbukwe kuwa Michael Jackson alizaliwa mwaka 1958 na kufariki dunia mwaka 2009. Alitamba na nyimbo zake kama vile Smooth Criminal, Thriller, Will You Be There.