Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matovolwa: Wasanii wa sasa ujuaji mwingi

Muktasari:

  • Mwigizaji Lumole Matovolwa ‘Kobisi’ amesema waigizaji wengi wa sasa wamejaa ujuaji kutokana na kutopita kwenye vikundi vya sanaa vinavyofundisha maadili kwa wasanii.

Dar es Salaam. Mwigizaji Lumole Matovolwa ‘Kobisi’ amesema waigizaji wengi wa sasa wamejaa ujuaji kutokana na kutopita kwenye vikundi vya sanaa vinavyofundisha maadili kwa wasanii.

“Vikundi vinalea  kwa hiyo ni muhimu, kwa sababu kuna utofauti kati ya wasanii waliokuja baada na kabla ya mwaka 2000. Ukimuweka msanii ambaye unasema wa zamani unaona wapo tofauti. Mmoja utakuta mstaarabu alafu mwingine atajifanya mjuaji.

“Makundi yalikuwa yanafundisha adabu, sanaa na kila kitu wanakuandaa jinsi ya kuwa staa. Sasa hivi msanii unamkuta barabarani unavutiwa na umbo lake unampa script anafanya. Ni tofauti na zamani ndiyo maana wasanii wengi siku hizi wanashindwa kujiumba kutokana na stori,”anasema

Anasema licha ya hayo kazi ya sanaa ya maigizo kwa sasa zinapanda kwani malipo ya waigizaji wa zamani ni tofauti na sasa.

“Nikifikiria nyuma filamu ya kwanza ‘Girlfriend’ nililipwa Sh 35000, na nilicheza ‘sini’ nyingi. Lakini sasahivi ‘sini’ moja huwezi kunilipa pesa ile. Siku hizi watu wanalipana mpaka Sh 30 milioni kwa hiyo tasnia imepanda 

“Kikubwa tukiacha ubinafsi tunaweza tukavuka mipaka zaidi kila mtu tumkubali katika eneo lake. Umimi ndiyo unafanya sisi tudumae. Wakenya wanatusumbua  tubadilike,”anasema