Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa waliong'ara tuzo za Trace 2025

Muktasari:

Licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa za kiufundi kwenye tamasha hilo, zilizopelekea Trace kushindwa  kurusha matangazo ya moja kwa moja 'Live', lakini baadhi ya wasanii walipata nafasi ya kutumbuiza kama vile Diamond Platnumz, Zuchu, Nandy, Rema, Marioo, Bien na wengine. 

Zanzibar. Usiku wa  Februari 26, 2025 limefanyika tukio kubwa la ugawaji wa tuzo za Trace Music Award lililofanyika Zanzibar kisiwani Unguja. Huku likiwakutanisha  wasanii  na wadau mbalimbali wa muziki duniani.

Licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa za kiufundi kwenye tamasha hilo, zilizopelekea Trace kushindwa  kurusha matangazo ya moja kwa moja 'Live', lakini baadhi ya wasanii walipata nafasi ya kutumbuiza kama vile Diamond Platnumz, Zuchu, Nandy, Rema, Marioo, Bien na wengine. 

Hata hivyo, tuzo hizo ambazo jana zilifanyika kwa mara ya pili tangu kuanzishwa kwake na mara ya kwanza nchini Tanzania ziliwaingiza baadhi ya wasanii katika ushindi.

Washindi wa Trace Music Awards 2025


Rema

Msanii aliyeng'ara zaidi kwenye usiku huo ni Rema ambaye aliondoka na tuzo tatu kutoka kwenye vipengele tofauti tofauti.
Rema alinyakua tuzo ya  ambavyo ni  Albamu Bora ya Mwaka kupitia albamu  yake ya Heis, iliyotoka Julai, 24, 2024. Ikiwa na jumla ya nyimbo 11.

Pia  alishinda kupitia kipengele cha Video Bora ya Mwaka, imeshinda video ya wimbo wa DND. Ambayo iliongozwa na Meji Alabi.

Aidha msanii huyo akashinda tena kipengele cha Msanii Bora wa Kiume. Kwa  hiyo Rema alinyakua tuzo tatu na kuibuka kinara kwenye tuzo.

Licha ya kuwa kinara, msanii huyo wa Nigeria alipata nafasi ya kutumbuiza wimbo wake wa uitwao ‘Ozeba’ kutoka kwenye albamu ya Heis.

Tyla

Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika  ilichukuliwa na mwanamuziki wa Afrika Kusini Tyla. Akiwashinda wasanii kama Makhadzi (Afrika Kusini), Chelsea Dinorath (Angola),  Josey (Ivory Coast), Ayra Starr (Nigeria), Tems (Nigeria), Yemi Alade (Nigeria).


Diamond Platnumz

Naye nyota wa muziki nchini Diamond aliondoka na Tuzo ya Trace katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiafrika Ulimwenguni 'Best Global African Artist' . Katika kipengele hicho Diamond aliwapiku wasanii kama Burna Boy na Asake kutokea Nigeria.


Titom
 

Wimbo Bora wa Mwaka katika tuzo hizo za Trace umechukua ‘Tshwala Bam’ wa kwake Titom &Yuppe (Afrika Kusini). Akiwashinda Tyla  ‘Jump’ (Afrika Kusini), Tyler ICU  ‘Mnike’ (Afrika Kusini), Tamsir x Team Paiya ‘Coup du Marteau’ (Ivory Coast), Asake & Travis Scott ‘Active’ (Nigeria), Tems  ‘Love Me Jeje’ (Nigeria), Burna Boy ‘Higher’ (Nigeria), Rema & Shallipopi  ‘Benin Boys’ (Nigeria), na Diamond Platnumz  ‘Komasava’ (Tanzania).


Didi B

Mshindi wa tuzo ya msanii bora wa Hip-hop Trace Music Awards 2025 ni Didi B kutokea Ivory Coast. Akiwapiku  Nasty C (Afrika Kusini), Odumodublvck (Nigeria), Suspect 95 (Ivory Coast), Sarkodie (Ghana), Young Lunya (Tanzania) na  Maglera Doe Boy (Afrika Kusini).


Fally Ipupa

Aidha mwanamuziki Fally Ipupa  (DRC) ameshinda katika kipengele cha Mtumbuizaji Bora wa Moja kwa Moja (Best Live Perfomance). Akiwashinda Ayra Starr (Nigeria), Burna Boy (Nigeria), Tyla (Afrika Kusini), Yemi Alade (Nigeria), Didi B (Ivory Coast), na Diamond Platnumz (Tanzania)

Tuzo za Ukanda/ Regional Awards
 

Bien 

Kutoka nchini Kenya, Bien ameshinda kipengele cha Msanii Bora Afrika.

Bien ameshinda tuzo hiyo akiwapiga chini Diamond Platnumz (Tanzania), Jushua Baraka (Uganda), Harmonize (Tanzania), Rophnan Ethiopia, Marioo (Tanzania), Zuchu (Tanzania), Nandy (Tanzania).

Nandy

Nandy ameshinda tuzo ya Msanii Bora Tanzania. Tuzo hiyo ameshinda mbele ya wasanii wengine kutokea Bongo ambao ni Mbosso, Diamond Platnumz (Tanzania) Zuchu (Tanzania) Marioo (Tanzania) Alikiba (Tanzania) Jux (Tanzania) Harmonize (Tanzania).

Ayra Staar  

Tuzo ya Msanii Bora Afrika Magharibi, Trace Music Awards 2025, ilienda kwa mwanadada Ayra Staar  akiwashinda Seyi Vibez (Nigeria), Adekunle Gold (Nigeria), Tems (Nigeria), Chike (Nigeria), Simi (Nigeria), KiDi (Ghana).


Tyler ICU

Msanii Bora Afrika Kusini kupitia tuzo za Trace Music Awards ameshinda Tyler ICU (Afrika Kusini)  akiwapiku Titom & Yuppe (South Africa), De Mthuda (South Africa), Inkabi Zezwe (South Africa), Dlala Thukzin (South Africa), Tyla (South Africa), Uncle Waffles (South Africa)