Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Aunty Ezekiel, Kusah tumuelewe hivyo tu!

Muktasari:

  • Kusah aliyetoka kimuziki na wimbo wake, Kelele (2019) akiwa na mpenzi wake wa zamani Ruby, kisha kuwania Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2021 kama Msanii Bora Chipukizi, tangu wakati huo ameendelea kuonyesha uwezo katika uimbaji na hata uandishi.

Dar es Salaam. Kwa kiwango fulani tunaweza kusema uhusiano wa Kusah na Aunty Ezekiel umechangia kuupaisha muziki wa mwimbaji huyo wa Bongofleva, na hadi sasa akiwa katika orodha ya mastaa wanaofanya vizuri kwa kiasi chake katika kiwanda hicho.

Kusah aliyetoka kimuziki na wimbo wake, Kelele (2019) akiwa na mpenzi wake wa zamani Ruby, kisha kuwania Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2021 kama Msanii Bora Chipukizi, tangu wakati huo ameendelea kuonyesha uwezo katika uimbaji na hata uandishi.

Ni hivi karibuni Kusah ameachia wimbo mpya, Kama Sio (2026) akishirikiana na staa wa Konde Music Worldwide, Harmonize ikiwa ni mara ya kwanza kwa wawili hao kufanya kazi pamoja.

Wimbo huo uliotayarishwa na Cukie Daddy, umechanganya sauti laini zenye hisia, mashairi ya kugusa moyo, pamoja na mdundo tulivu wa Bongofleva unaobeba ujumbe mzito wa mapenzi na uaminifu.

Tayari umeanza kupata idadi kubwa ya watazamaji na wasikilizaji katika mitandao kama YouTube, Boomplay Music na Audiomack, kitu kinachothibitisha nguvu ya ushawishi walionayo wasanii hawa na pia ubora wa kazi yenyewe.

Katika video yake iliyoongozwa na Director Fole X, mshindi wa TMA 2023, ameonekana mpenzi wa Kusah na mzazi mwenzie, Aunty Ezekiel, vilevile mchumba wa Harmonize, Kajala Masanja, ambaye inakuwa ni video ya tatu kufanya na mpenzi wake huyo.

Licha ya ukosolewaji waliokumbana nao katika mitandao ya kijamii, bado haiondoi ukweli kwamba wamefanya kazi nzuri. Director Fole X ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya All Africa Music Awards (AFRIMA) 2025, mara zote kazi yake huwezi kuitilia shaka hata kidogo.

Kwa ujumla hiyo inakuwa video ya nne kwa Kusah kufanya na Aunty Ezekiel baada ya I Wish (2021), Mama Lao (2021) na Blessings (2025), ambayo ni kwa ajili ya mtoto wao wa pili ambaye pia Kusah kamwimbia wimbo, Ukiniita (2025) unaozungumzia kuzaliwa kwake.

Jambo hili ndilo limefanya video hii mpya kukosolewa, watu wanahoji kwani Kusah na Harmonize wanafanya muziki kwa ajili ya wapenzi wao tu au mashabiki? Kama ni kwa ajili ya mashabiki, basi wafanye zaidi ya hapo, yaani kutoa nafasi kwa warembo wengine.

Hata hivyo, kwa upande wake Kusah kufanya kazi na Aunty Ezekiel ni biashara inayolipa vizuri katika muziki wake kwani wimbo wake wenye mafanikio zaidi katika majukwaa yote ya kidijitali mrembo huyo alihusika tangu mwanzo.

Wimbo huo ni I Wish (2021) ambao tunaweza kusema ndio uliompa Kusah umaarufu mkubwa zaidi. Kabla ya kuachiwa kwa video yake, kulisambaa mtandaoni picha na video za wawili hao ambazo zilidaiwa wamefunga ndoa lakini ukweli ni kwamba ndipo walikuwa wanashuti.

Video ilipotoka ikafanya vizuri sana na hadi sasa ikiwa imetazamwa (views) zaidi ya mara milioni 20 YouTube, na hakuna video yake nyingine ambayo imefikia hata nusu ya namba hizo, hivyo Kusah anapofanya kazi na Aunty Ezekiel tunapaswa kumwelewa kwa upande huo.

Na ukizingatia hiyo ndio ilikuwa video ya kwanza kwa wawili hao kushirikiana na ikampa matokeo makubwa kiasi hicho, hivyo kwa hali ya kawaida tu asingekubali kuishia hapo, na ndio sababu ameendelea kushuti naye hadi sasa zimefika jumla ya video nne.

Wakati akitangaza ujio wa wimbo wake huu mpya, Kama Sio (2026), alisema endapo hautafanya vizuri, basi atapumzika muziki kwa kipindi cha miaka mitatu, kauli ambayo ilifanya wengi kujiuliza kwani wimbo huu una kitu gani maalumu hadi kufikia kusema maneno ya kishujaa hivyo.

Lakini kwa Kusah alijua wimbo wake una video kali na ndani yake yupo Aunty Ezekiel na Kajala, hivyo kivyovyote vile itapata mapokezi mazuri kutokana na ushawishi wa waigizaji hao, na kubwa zaidi rekodi nzuri walizonazo katika video za muziki ambazo walitokea.

Ikumbukwe Kajala kwa mara ya kwanza kuonekana katika video ya Harmonize ilikuwa ya wimbo, Nitaubeba (2022) ambao umeshatazamwa YouTube mara milioni 44, ikiwa ni video ya tano kwa Harmonize kufanya vizuri zaidi katika mtandao huo.


Huko ndipo Kusah alipokuwa anatazama katika kolabo yake hii na Harmonize, na tunaweza kusema amefanikiwa kwa sababu tayari video hiyo imeshatazamwa mara milioni 2 YouTube ikiwa ni wiki moja tangu kuachiwa kwake, hivyo hatutegemei kumwona akipumzika muziki kwa miaka mitatu kama alivyosema.

Utakumbuka Kusah ambaye ukaribu wake na Aunty Ezekiel ulianzia Instagram kisha wakaja kuwa wapenzi na sasa wazazi wa watoto wawili, bado hajatoa albamu ila amefanikiwa kuachia Extended Playlist (EP) mbili, Romantic (2022) na Bumbuli Boy (2025).

Na kipindi cha uhusiano wake na Ruby, ndipo Kusah alimwandikia wimbo wake maarufu, Ntade (2018) ambao ulifanya vizuri sana na kumrudisha Ruby katika muziki baada ya ukimya mrefu.  

Vilevile walifanikiwa kutoa nyimbo tatu pamoja ambazo ni Chelewa (2018), Kelele (2019) na Nadondosha (2019). Baada ya nyimbo hizo ukawa mwisho wa penzi lao, kisha Kusah akaenda kwa Aunty Ezekiel ambaye pia wanashirikiana katika kazi zake ila mtindo tofauti.