Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aunt Ezekiel sasa ni Rahma afunga ndoa na Kusah

AUNT Pict

Muktasari:

  • Baada ya kubadili dini, Aunt Ezekiel sasa anaitwa Rahma, jina ambalo alilitumia kwenye ndoa yake ya kwanza mwaka 2012 alipooolewa na mfanyabiashara, Sunday Dimonte.

Dar es Salaam. Nyota  wa filamu za Kibongo, Aunty Ezekiel, amebadili dini  kutoka Ukristo na kuwa Muislam baada ya kuolewa na msanii wa Bongofleva, Kusah.

Baada ya kubadili dini, Aunt Ezekiel sasa anaitwa Rahma, jina ambalo alilitumia kwenye ndoa yake ya kwanza mwaka 2012 alipooolewa na mfanyabiashara, Sunday Dimonte.

Kwa mujibu wa Kusah,  amemuona Aunt Ezekiel miezi kadhaa iliyopita kwa kufuata taratibu zote za dini ya Kiislamu, ambapo ndoa hiyo ilikuwa kimya kimya bila ya kufanya sherehe.

"Kwa sasa Aunt Ezekiel anaitwa Rahma, amebadili dini na tukafunga ndoa kimya kimya, tulifuata taratibu zote za dini ya Kiislamu, sasa rasmi ni mke wangu ambaye amenizalia watoto wawili," amesema Kusah.

AUN 01

Kusah alitoa sababu ya kufunga ndoa kimya kimya, bila ya sherehe kubwa kama baadhi ya wasanii wengine walivyofanya ambapo amesema ni kutokana na kuona hatua kubwa ya kufunga ndoa ilitimia hivyo sherehe haikuwa na ulazima sana.

"Hapana, sikutaka kufanya sherehe kubwa, sababu lile ambalo tumekusudia kulifanya la kufunga ndoa ndio lilikuwa muhimu sana kuliko sherehe, hivyo hakukuwa na ulazima sana kufanya sherehe," amesema Kusah.

Kwa upande wa Aunt Ezekiel, Mwananchi ilimuuliza sababu ya kurudia jina ambalo alishawahi kutumia kwenye ndoa yake ya kwanza ambapo amesema:

"Sikuona kuhangaika kutafuta jina lingine la Kiislamu wakati tayari nilishakuwa na jina hapo awali pindi nilipoolewa, na pia jina la Rahma nalipenda sana, niseme tu sikuwa na wazo kabisa na ndoa tena, lakini nikawa tayari sababu ya kuona niliyekuwa naye ni sehemu sahihi kwangu, sikuweza kupinga pale aliponiambia anataka tufunge ndoa, jamani Kusah ni mwanaume haswa yaani ni baba bora na sio bora baba."

AUN 02

Hii ni ndoa ya pili kwa Aunt Ezekiel kufunga kimyaa kimya, ya kwanza ilikuwa mwaka 2012 nchini Dubai alipofunga na mfanyabiashara, Sunday Dimonte.

Mwaka 2014, ndoa hiyo ilivunjika na Aunt Ezekiel kurudi kwenye dini yake ya Ukristo.

Kwa upande wa Kusah na Aunt Ezekiel, toka waanzishe mahusiano ya kimapenzi, hadi sasa wana miaka mitano na  wamefanikiwa kupata watoto wawili wa kiume na wa kike.

Wawili hao kabla ya kuanzisha mahusiano hayo, tayari walishapata watoto na mahusiano yao mengine, ambapo Kusah alipata mtoto na msanii wa Bongofleva, Ruby, huku Aunt Ezekiel akipata mtoto na mcheza shoo wa msanii wa Bongofleva, Diamond aitwaye Mose Iyobo.