Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesho ya nyimbo za wasanii wa kizazi kipya ni kitendawili

Muktasari:

  • Swali linakuja kwa sababu kila wasanii wa kisasa wanaporudia ngoma za zamani, zinakuwa ngoma kali sana huku sababu kuu zikiwa mbili kwanza wasanii wa kisasa wana vipaji vikubwa sana, hivyo wanaporudia ngoma wanazitia mbwembwe na machejo yanayofanya ngoma ipendeze

Dar es Salaam. Kila ninaposikia nyimbo za wasanii wa zamani zikirudiwa sasa kitu cha kwanza kuja kichwani kwangu ni swali la “Wasanii wa miaka 10, 15 ijayo watafanya remix ya nyimbo gani?”

Swali linakuja kwa sababu kila wasanii wa kisasa wanaporudia ngoma za zamani, zinakuwa ngoma kali sana huku sababu kuu zikiwa mbili kwanza wasanii wa kisasa wana vipaji vikubwa sana, hivyo wanaporudia ngoma wanazitia mbwembwe na machejo yanayofanya ngoma ipendeze.

Lakini pili, ngoma za zamani zimetengenezwa kwa midundo mizuri sana. Kama huamini kaisikilize Yule remix ya AY iliyofanywa na Marioo. Yaani nyimbo za zamani zina midundo yenye ubunifu, midundo kutoka kichwani kwa prodyuza mwenyewe.

Midundo ambayo haijafanyiwa sampling kutoka kwenye ngoma za watu wengine. Ndiyo maana zamani ilikuwa ni ngumu sana kukuta nyimbo zimefanana biti, ukiona hivyo ujue nyimbo ilikopiwa kwa makusudi.

Ukiunganisha ubora, ubunifu upekee wa biti za zamani na vipaji vikubwa vya wasanii wa kisasa mara nyingi mambo huwa mwake mwake. Kama unataka ushahidi zaidi kuhusu hili kasikilize albamu ya P Funk Majani inayoitwa Majani na humo ndani imechukuliwa midundo ya ngoma 14 zilizotengenezwa na P Funk kitambo hicho, zikapewa touch ya kisasa kisha rappers wa kisasa kama Young Lunya, Connboi, Country Wizzy na wengine wakaimba humo. Ilikuwa na ladha tofauti sana.

Swali la wasanii wa miaka 10, 15 ijayo watafanya remix ya wimbo gani linakuja kwa sababu ukweli ni licha ya kuwa muziki wetu umekuwa sana na wasanii wetu wana vipaji sana lakini ubunifu kwenye uandaji wa muziki umepungua sana.

Wasanii wengi wamekuwa wakitoa nyimbo za kufanana midundo. Nyimbo za kufanana melody. Yaani siku hizi, msanii mkubwa kama Diamond akitoa ngoma kuna asilimia kubwa ya ngoma hiyo kuwa wazo lilichukuliwa kutoka kwenye ngoma nyingine ya msanii mwingine wa Nigeria au Afrika Kusini.

Pia, wasanii wengi wanaimba muziki ule ule, Amapiano, ambao kitaalamu ni muziki mgumu sana kutofautisha kati ya biti na biti. Pia biti zake nyingi zinafanana mno hata kama hazijaibwa.

Kwa kifupi, asilimia kubwa ya muziki wa kisasa hauna thamani kubwa ya kisanii ambayo mara nyingi ndiyo inayowachochea na kuwashawishi wasanii kutaka kurudia nyimbo za zamani.

Kwa mfano wimbo unaovuma kwa sasa ni Komasava wa Diamond. Nambie, kwa kuusikiliza unadhani ni muziki ambao miaka 10 mbele kuna msanii atataka kuufanya remix? Pengine remix pekee za kutarajia za Komasava ni sasa ambazo nyingi zinachochewa wasanii wanaotaka ifanyike remix, kutaka kuteleza na upepo wa ngoma hiyo.

Niwape pole wasanii wa kisasa, miaka ijayo itabidi muumize kichwa zaidi maana hakutakuwa na ngoma za kurudia.