Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hata kina Beyonce, Rihanna wana lebo zao

Muktasari:

  • Hata wanamuziki wakubwa kama Beyonce, Rihanna ambaye kwa sasa ni bilionea, wana lebo zao lakini sio maarufu sana maana kwa sehemu kubwa zinafanya kazi nchi nyingine ambazo ndizo zina nguvu kubwa katika tasnia

Marekani. Tofauti na Tanzania, rekodi lebo nyingi za wasanii hasa nje ya bara la Afrika, zimekuwa na utamaduni wa kuingia makubaliano ya kufanya kazi na lebo kubwa ambazo zina wingo mpana wa kusambaza kazi na masoko.

Hata wanamuziki wakubwa kama Beyonce, Rihanna ambaye kwa sasa ni bilionea, wana lebo zao lakini sio maarufu sana maana kwa sehemu kubwa zinafanya kazi nchi nyingine ambazo ndizo zina nguvu kubwa katika tasnia.


Beyonce - Parkwood Entertainment, LLC

Parkwood Entertainment, LLC ni kampuni ya usimamizi, utayarishaji na rekodi lebo iliyoanzishwa na mwimbaji wa Marekani, Beyonce Knowles mwaka 2010. Hata hivyo, ilianza kama kitengo cha utayarishaji wa filamu na video mwaka 2008.

"Nilianzisha kampuni yangu nilipoamua kujisimamia, ilikuwa muhimu kwamba nisiende kwenye kampuni kubwa ya usimamizi, nilihisi ninataka kufuata nyayo za Madonna na kuwa mtu mwenye nguvu na kuwa na himaya yangu mwenyewe. Kuonyesha wanawake wengine unapofikia hatua hii sio lazima uende kusaini na mtu mwingine," alisema Beyonce.

Beyonce alipata umaarufu tangu miaka 1990 akiwa na kundi la Destiny's Child lililosambaratika rasmi mwaka 2005, alianza kufanya muziki kama solo baada ya kutoa albamu yake ya kwanza, Dangerously in Love (2003), na hadi sasa ameshinda tuzo 35 za Grammy.


Madonna - Maverick

Maverick ilikuwa kampuni ya burudani ya Marekani iliyoanzishwa mwaka 1992 na Madonna. Frederick DeMann na Veronica "Ronnie" Dashev, ndani yake ikawepo Maverick Records iliyokuwa ikimilikiwa na kuendeshwa na Warner Music Group.

Madonna akawa mmoja wa wasanii wa kwanza wa kike kuwa na lebo na mmoja wa wanawake wachache kuendesha kampuni yake ya burudani, Madonna na Dashev waliondoka katikati kampuni hiyo mwaka 2004 baada ya kesi kati ya Maverick na Warner Music.

Ikumbukwe Madonna aliyevuma sana na wimbo wake, La Isla Bonita (1986), anakadiriwa kutengeneza Dola1.2 bilioni na ndiye mwanamuziki wa kike aliyelipwa fedha nyingi zaidi kila mwaka katika miongo minne, kuanzia mwaka 1980 hadi 2010.


Katy Perry - Unsub Records

Unsub Records ambayo awali ilitambulika kama Metamorphosis Music ni rekodi lebo inamilikiwa na Capitol Music Group na ilianzishwa mwaka 2014 na mwimbaji wa Marekani, Katy Perry, huku Ferras akiwa msanii wa kwanza kusainiwa.

Julai 2017, Perry alimsaini Cyn ambaye alitambulishwa kwake na DJ Skeet Skeet baada ya kukutana naye kwenye ziara ya Perry, California Dreams Tour, na Mei 2021, Perry alimsaini Michael J. Woodard ambaye alishiriki msimu wa 16 wa American Idol.

Katy Perry, mkali wa kibao, Roar (2013) ambacho video yake imetazamwa YouTube zaidi ya mara bilioni 4.1, alitajwa na Billboard kama mwanamuziki wa kike aliyelipwa fedha nyingi zaidi duniani mwaka 2015 na 2018, pia kuwa mmoja wa wasanii wakubwa wa pop wa karne ya 21.


Rihanna - Westbury Road Entertainment

Baada ya kumalizika mkataba wake wa miaka 10 na Def Jam Recordings mwaka 2015, Rihanna alianzisha lebo yake, Westbury Road Entertainment ikiwa na makubaliano ya ushirikiano na Roc Nation ya Jay Z.

Aliamua kiita Westbury Road 'Entertainment' kama kutoa heshima ya eneo ambalo alikulia huko Barbados, albamu yake ya nane, ANTI iliyotoka Januari 28, 2016 ndiyo ya kwanza kuachiwa chini ya lebo hiyo na tangu wakati huo hajatoa albamu nyingine.

Ukubwa wa Rihanna katika muziki ulikuja baada ya kutoa albamu yake ya tatu, Good Girl Gone Bad (2007) na kushinda Grammy kwa mara ya kwanza, hadi sasa akiwa ameuza rekodi zaidi ya milioni 250 duniani kote, utajiriwa wake unakaridiwa kufikia Dola1.4 bilioni.