Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harmonize amchangia Ibrah atoke Konde Gang

KONDE Pict

Muktasari:

  • Harmonize amesema Lebo ni biashara kama zilivyo zingine na Ibrah anatakiwa kulipa pesa anazodaiwa ili mambo mengine yaendelee.

Baada ya kuibuka kwa malalamiko kutoka kwa msanii wa Konde Gang, Ibrah akiomba msaada kwa Watanzania wa Sh1 Bilioni ili aweze kutoka katika lebo hiyo, bosi anayemsimamia, Harmonize ameibuka na kuthibitisha madai hayo huku akimchangia.

Harmonize amesema Lebo ni biashara kama zilivyo zingine na Ibrah anatakiwa kulipa pesa anazodaiwa ili mambo mengine yaendelee.

Sambamba na hilo Harmonize amechangia kiasi cha Sh100,000 Ibraah ili aweze kufanikisha kulipa deni analodaiwa na Konde Gang.

Harmonize ameandika “Namuelewa sana Ibraah, kwani hata mimi nimewahi kupitia “Situation" kama hiyo na nililipa kiasi nilichodaiwa hivyo Ibraah pia anatakiwa kulipa."

Konde Boy aliongeza kwa kuandika kuwa, mwamba Ibrah ana roho mbaya na wivu kwani hata siku anaposti jambo la madai ilikuwa ni siku ambayo mitandao ilichafuka kwa kuzungumzia matukio katika sherehe ya kumbukizi ya kuzaliwa Amara mtoto wa Paula na Marioo ambapo Harmonize alikuwa kwenye headline matukio yake na Kajala ambayo ilisemekana wamerudiana.

“Nimemchunguza sana mdogoangu Chinga nimegundua ana roho mbaya na kama sio ibilisi amempanda kichwani, maana hata siku aliyo post na kusema namdai 1.B niile siku ya Birthday ya mjukuu wangu amara, yani mimi na kipenzi change tuna trend, kifupi alisikia wivu guys sijamuomba chinga bilioni ila mkataba alio sign na lebo unasema ikitokea watu wanataka kumnunua wenye malengo makubwa zaidi ya Konde Gang. Pengine tunaweza tofautiana kipato inatakiwa ailipe label Konde Gang 1.B ili wawasaidie vijana wengine na nilimwambia nitabaki kuwa kaka yako na Konde Gang chama lako this guy have 2py mchangieni nililipa kwa kukopa.