Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond ataja sababu ya kuvaa kimasai kwenye ‘Komasava’

Dar es Salaam. Baada ya kuwepo na minong’ono kupitia mitandao ya kijamii kwa baadhi ya mashabiki wakihoji kwanini Diamond Platnium aliamua kuvaa vazi la Kimasai katika video yake na kwanini asingevaa mavazi mengine kama Kitenge, staa huyo anayeshika namba moja YouTube kupitia ngoma yake ya ‘Komasava Remix’ amefunguka sababu ya yeye kuvaa vazi hilo.

Kufuatiwa na video inayosambaa mitandaoni ambayo imepostiwa dakika chache zilizopita imemuonesha msanii huyo akitolea ufafanuzi sababu ya kushoot ngoma hiyo mkoani Arusha na kuvaa mavazi hayo ni kutokana na nchi nyingi za Afrika kuvaa vazi hilo.

“Tupo Monduli Arusha na kilichotuleta huku ni kushoot nyimbo ya ‘Komasava’ kwenye ile party ya ‘Habari Gani’ kwanini tumeamua kushoot huku na kwanini tumeamua kuvaa Kimasai ni kwa sababu katika hizi nchi tatu au nchi za Afrika Mashariki nyingi zinapendelea kuvaa Kimasai na vilevile pia ni nchi zinazoongea Kiswahili kwa hiyo tulibidi tuvae vazi linalowakilisha Kiswahili na vazi hilo ni Kimasai”

Hii si mara ya kwanza kwa Diamond ‘Simba’ kuvaa vazi la kimasai utakumbuka kuwa mwaka 2021 alitinga na vazi kama hilo katika usiku wa tuzo za BET zilizofanyika Microsoft Theatre, Los Angeles, Marekani.

Kichupa hicho kinachoendelea kutamba mjini mpaka kufikia sasa kinazaidi ya watazamaji milioni 4 kupitia mtandao wa YouTube zikiwa na siku nne tu tangu kuachiwa kwake.