Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Basilla:Kifo cha Anko Hashim tumepoteza nguzo ya tasnia ya urembo

Muktasari:

  • Ballisa amesema Lundenga alimuuzia leseni za mashindano ya Miss Tanzania tangu mwaka 2018.

Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Look inayoendesha mashindano ya kumsaka Miss Tanzania, Basilla Mwanukuzi ameelezea namna marehemu Hashim Lundenga alivyomuachia kijiti cha kuongoza mashindano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kuaga mwili wa Lundenga nyumbani kwake Bunju B. Ballisa amesema Lundenga alimuuzia leseni za mashindano ya Miss Tanzania tangu mwaka 2018.

"Kwa kweli tumepata msiba mkubwa niseme tumepoteza nguzo ya tasnia ya urembo. Anko Hashim ni mlezi na muasisi wetu mimi mwenyewe ni Miss Tanzania mwaka 1998 ambaye nimetokana na malezi yake.

“Kwahiyo nilipitia jukwaa hili hadi mimi kutambulika katika jamii. Lakini kama mnavyofahamu mashindano ya Miss Tanzania yanamilikiwa na watu binafsi ni biashara kwa hiyo  anko Hashim alivyoona amechoka  akaniachia,”amesema Ballisa

Amesema Lundenga amefanya kazi kubwa kuipambania tasnia ya urembo Tanzania hadi kutambulika  katika ngazi  ya mashindano ya dunia 'Miss World'.

"Tasnia ya urimbwende inabadilika kipindi chake. Yeye alikuwa na kazi kubwa ya kuitambulisha sanaa hii ili ieleweka kwa watu waelewe sanaa ni nini, urembo ni nini. Mashindano ni nini lakini pia nyakati zake alipigania isiishie tu Tanzania iende katika kinyang'anyiro cha kimataifa kwenye mashindano ya Miss World.

“Kwahiyo alikuwa na kazi ya kutambulisha sanaa kuweka misingi kutengeneza sheria kanuni. Lakini pia mpaka serikali yenyewe kuikubali sanaa. Walikuwa hawaelewi wanasema haya mashindano ni kinyume na mila zetu wakapiga marufuku,”amesema

Amesema kwa juhudi za  Hashim serikali ikaipokea Miss Tanzania kwa mikono miwili. Kupitia Basata wakatengeneza kanuni ambazo zimeendelea kuboreshwa ili mashindano yawe bora zaidi.

Ameongezea  licha ya kuwa nyakati zimebadilika na matamasha yameongezeka lakini bado jukwaa la  Miss Tanzania ni ndoto ya wasichana wengi nchini.

"Nyakati zimebadilika zamani tamasha la Miss Tanzania lilikuwa pengine ndio  pekee watu wanajua. Siku hizi kuna mambo mengi kuna matamasha ya muziki. Watu wana machaguo mengi lakini bado jukwa la Miss Tanzania limeendelea kuwa ndoto kwa binti wa kike,” amesema 

Aidha, amesema mwaka huu 2025 inaandaliwa fainali ya Miss Tanzania baada ya kutofanyika mwaka 2024 kutokana na majukumu yake ya kiserikali.

" Kama mnafahamu mwaka jana mashindano yalifanyika ngazi ya awali, tumeona sasa tuandae fainali ambayo haikuandaliwa. Kama mnavyofahamu mimi nilikuwa kwenye majukumu ya kiserikali. Niliteuliwa na Rais kuwa mkuu wa Wilaya ya Korogwe kwa hiyo nilikuwa nimeachia watu wasimamie.

“Lakini safari hii nipo kwa hiyo tunaandaa tamasha kubwa, shindano ambalo litafanyika Agosti. Hivyo tutampata Miss Tanzania 2025" amesema Basila.