Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asake aingiza nyimbo 50 Billboard

Muktasari:

  • Asake mwenye albamu tatu hadi sasa ameingiza jumla ya nyimbo 50 Billboard na kumpita Burna Boy ambaye alikuwa anashikilia rekodi hiyo kwa kipindi kirefu

Nigeria, Staa wa Afrobeat kutoka Nigeria, Asake, 29, ameweka rekodi kama mwanamuziki pekee Afrika aliyeingiza nyimbo nyingi katika chati ya Billboard U.S. Afrobeats Songs ambayo ilizinduliwa rasmi Machi 2022.

Asake mwenye albamu tatu hadi sasa ameingiza jumla ya nyimbo 50 Billboard na kumpita Burna Boy ambaye alikuwa anashikilia rekodi hiyo kwa kipindi kirefu.

Chati ya Billboard U.S Afrobeats Songs inatoa orodha ya nyimbo 50 kutoka Afrika ambazo ni maarufu Marekani na inapangwa kwa jinsi wimbo husika unafanya vizuri upande wa kusikilizwa na mauzo kwenye majukwaa makubwa ya mtandaoni.

Utakumbuka Asake ambaye amevuma na nyimbo zake kama ‘Lonely At the Top’ na ‘Sungba’, alishinda tuzo ya AFRIMA kama Msanii Bora Chipukizi 2020 na amewania tuzo kubwa za kimataifa kama Grammy, BET, NAACP n.k.

Rekodi hiyo ya Asake inakuja baada ya albamu yake mpya, Lungu Boy (2024) iliyotoka mwezi huu ikiwa na nyimbo 15, kuingiza nyimbo 9 katika chati hizo maarufu Afrika.

Albamu hiyo iliyotoka chini ya rekodi lebo za YBNL Nation na Empire Distribution, imeshirikisha wasanii wakali kama Wizkid, Travis Scott, Stormzy, Central Cee na Ludmill huku watayarishaji wakiwa ni P.Priime, Magicsticks, Mike Dean, Sarz na Sak Pase.

Wimbo wake ‘Active’ akimshirikisha Travis Scott, rapa kutoka Marekani ndiyo umeshika nafasi ya juu zaidi ukifuatiwa na ‘MMS’ akiwa na Wizkid, kisha ‘Mood’, ‘Fuji Vibes’ na ‘Suru’ akiwa na Stormzy.

Vilevile albamu hiyo ambayo imeweka rekodi kama albamu ya kwanza kutoka Nigeria kushika nafasi za juu zaidi chati ya Apple Music Marekani na kukamata namba Apple Music Uingereza, pia imeingia Billboard 200, chati maalumu kwa ajili ya albamu.

Mafanikio haya ni mwendelezo wa kile ambacho albamu zake mbili za mwanzo zilifanya katika chati mbalimbali. Albamu hizo ni Mr. Money With The Vibe (2022) na Work of Art (2023) ambazo zote ziliingia Billboard 200 na kushika namba 66.

Ikumbukwe Machi 29, 2022 ndipo chati ya kwanza ya Billboard U.S Afrobeats Songs ilitoka ambapo wimbo ‘Love Nwantiti’ wake Ckay ulishika namba moja, ukifuatiwa na ‘Peru’ wake Fireboy DML, kisha ‘Essence’ wa Wizkid. Wasanii wote hao wanatoka Nigeria.