Usher ataka kupita anga za Burna Boy, Davido, Asake

Muktasari:
- Hii inakuja baada ya kuvutiwa na uimbaji wa wasanii kutoka nchini Nigeria, ambapo tayari ameshafanya ‘kolabo’ na mwanamuziki Burna Boy na Pheelz katika album yake mpya ya ‘Home Coming’.
Marekani. Mkali wa R&B, kutoka nchini Marekani, Usher ameweka wazi kuwa anataka kuwa sehemu ya muziki wa Afrobeat.
Hii inakuja baada ya kuvutiwa na uimbaji wa wasanii kutoka nchini Nigeria, ambapo tayari ameshafanya ‘kolabo’ na mwanamuziki Burna Boy na Pheelz katika album yake mpya ya ‘Home Coming’.
Kupitia mahojiano yake na Apple Music, Usher ameeleza kuwa ana mpango wa kufanya ‘kolabo’ zaidi na wasanii wa Nigeria na kupeleka utamaduni wa Afrika bara la Amerika kutokana ngoma zao kuwa maarufu duniani kote.
Ukiachilia mbali wasanii wa Nigeria, mkali huyo wa R&B kwa hapa Tanzania ameomba kufanya ‘kolabo’ na mwanamuziki Nandy kupitia wimbo wa ‘Dah’, ambapo mpaka sasa bado haijafahamika rasmi remix hiyo itaachiwa lini. Muziki wa Afrobeat au kwa jina lingine ‘Afrofunk’ ni aina ya muziki wa Kinaigeria ambao unahusisha mchanganyiko wa mitindo ya muziki wa kitamaduni wa Kiyoruba na Igbo.
Wakali wa muziki huo ni Davido, Burna Boy, Asake, Rema, Tiwa Savage na wasanii wengine kutoka Nigeria.