Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyeimba na Bob Marley afariki dunia

Muktasari:

Mwanamuziki wa Raggae kutoka Jamaica ambaye aliwahi kufanya kazi kwenye bendi ya Marehemu Bob Marley  kama 'bassist'  afariki dunia

Dar es Salaam: Aliyekuwa mwanamuziki wa nyimbo za #Raggae kutoka nchini Jamaica #AstonBarrett, maarufu kama ‘Family Man’ amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77.

Mwanamuziki huyo alipata umaarufu nchini humo na duniani kote akiwa kwenye Bendi ya #Upsetters, iliyokuwa chini ya mwanzilishi mmoja wa Reggae, Lee ‘Scratch’.

Pia mwaka 1994, alijiunga na bendi ya marehemu Bob Marley (Bob Marley and the Wailers) akiwa kama mpiga besi (bassist) wa bendi hiyo, alikuwa mmoja wa watu waliochangia sana kukua kwa Reggae ulimwenguni.

Barrett yupo kwenye kila albumu ya Bob ‘Wailers’, pamoja na kufanya kazi na wanamuziki maarufu kama Burning Spears, Peter Tosh.

Baadhi ya nyimbo maarufu ambazo aliwahi kuwemo akiwa kwenye bendi ya Bob Marley ni pamoja na  ”Get up Stand Up, Stir It Up, No Woman, No Cry na  Could You Be Love”.

Family Man alizaliwa mwaka 1946, Kingston nchini Jamaica na kufariki mwaka 2024, kutokana na matatizo ya kiafya aliyokuwa akipambana nayo kwa muda mrefu ambayo familia yake haikutaka kuyaweka wazi.

Taarifa za kifo chake zilitolewa na mtoto wake wa kiume aitwaye Barrett Jr Jumamosi iliyopita kupitia mitandao ya kijamii, ambapo aliandika, “ Kwa moyo mgumu tunatoa taarifa ya kufariki kwa mpendwa wetu Aston 'Familyman' Barrett baada ya kupambana na matibabu kwa muda mrefu."