Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alichofanya Alikiba hata CR7, Pogba walifanya

Muktasari:

  • Kwa zaidi ya siku nne sasa mitandaoni kumekuwa na majadiliano kuhusiana na mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Alikiba kuondoa logo ya mdhamini mkuu kwenye jezi ya Simba aliyoivaa wakati akitumbuiza kwenye uzinduzi wa jezi hizo.

Dar es Salaam. Wasanii na wachezaji maarufu mara nyingi hujikuta kwenye taharuki katika mitandao ya kijamii kutokana na baadhi ya matendo wanayafanya ambayo huenda yakawa ya kawaida lakini mbele ya jamii yakawa ya ajabu.

Kwa zaidi ya siku nne sasa mitandaoni kumekuwa na majadiliano kuhusiana na mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Alikiba kuondoa logo ya mdhamini mkuu kwenye jezi ya Simba aliyoivaa wakati akitumbuiza kwenye uzinduzi wa jezi hizo.

Kitendo hicho kiliwavuruga wengi kutokana na jina la ‘Betway’ kufutwa. Ambapo wadau mbalimbali wa muziki wamedai ilikuwa sawa kwa King Kiba kufanya hivyo kwani yeye ana makubaliano na klabu ya Simba hivyo hayahusiani na mdhamini mkuu wa timu huo. 

Wanadai kuwa alichofanya ni kulinda heshima na maslahi yake kama msanii. Hata hivyo wapo waliokuwa na mawazo hasi wakisema hakukua na sababu kwa msanii huyo kufanya hivyo. Licha ya maoni hayo ni vyema kufahamu kuwa Kiba siyo staa wa kwanza kufanya hivyo wapo na wengine.

Tukio kama hilo limewahi kufanywa na nyota wa Al Nasr Cristiano Ronaldo mwaka 2021 kwenye mashindano ya ‘Euro 2020’ wakati alipokuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari. Katika meza aliyofikia alikuta chupa mbili za Coca-Cola ambaye ndio alikuwa mdhamini mkuu katika michuano hiyo CR7 alizichukua na kuzishusha chini huku akichukua chupa ya maji na kuinyanyua juu.

Tukio hilo lilizua mijadala katika mitandao ya kijamii kwani alionekana kutopendelea bidhaa za kampuni hiyo huku mashabiki mbalimbali wakimpongeza kwa kusimamia heshima yake. Hata hivyo baada ya muda mchache kupita kampuni hiyo ilitoa taarifa kuwa kutokana na tukio hilo ilipoteza zaidi ya dola bilioni 4 huku bei ya hisa zao ikishuka kutoka karibu dola 56.10 hadi dola 55.22 kwa kila hisa.

Baada ya siku chache kupita naye mwanasoka Paul Pogba alijikuta katika sakata hilo ambapo baada ya mechi ya Euro 2020 kati ya Ufaransa na Ujerumani wakati alipoingia kwenye chumba cha mkutano na waandishi wa habari mezani alikuta chupa ya bia ya Heineken ambao walikuwa wadhamini wakuu katika mashindano hayo. Ndipo akaitoa na kuweka chini.

Kitendo hicho kilipongezwa na wengi katika mitandao ya kijamii hasa wale waliokuwa waislamu kwani ilielezwa kuwa Pogba alifanya hivyo kutokana na kuheshimu dini yake ambayo haikubali muumini kutumia pombe. 

Aidha kwa upande wa Heineken wao waliweka wazi tukio hilo halipoteza hisa zao licha ya mauzo kushuka kwani waliweka tamko kuwa chupa iliyowekwa mezani ilikuwa Heineken 0.0, yaani pombe isiyo na kilevi.

Ukiachana na Pogba, CR7 kwa Bongo naye mama mzazi wa msanii maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz. Alijikuta amezua mijadala katika mitandao ya kijamii baada ya video yake ikimuonesha akitupa chupa chini ya uvungu wa kochi baada ya kugundua kuna kamera zikimrekodi.

Tukio hilo lilizua mijadala huku wadau mbalimbali wakieleza kuwa mama mzazi wa msanii huyo alifanya kitendo hicho kwa lengo la kulinda jina la mwanaye lakini pia Diamond hakuwa na makubaliano na kampuni hiyo ya maji.

Hivyo basi staa anapohamisha chupa ya kinywaji chochote si jambo la dharau bali ni kwa ajili ya kulinda heshima na maslahi yake ya kibiashara.